DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Monday, January 20, 2014

MAMA WAWILI WASHUHUDIA JINSI MUNGU KWA KUPITIA MAOMBI YA NABII FLORA ALIVYOWASAIDIA KURUDIWA NA WAUME ZAO

MAMA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMREJESHA MUME WAKE NYUMBANI

Bwana Yesu asifiwe; Nabii Flora ni kiboko, ukimshukuru atazidi kukusaidia, ukizidi kuomba na yeye akiomba, Mungu atakubariki na wewe utafanikiwa. Mimi nimefanikiwa kwaajili ya Nabii Flora, nilikaa miaka 6 bila mume, mume alichukuliwa na kahaba alikuwa Bunju, lakini kutokana na madhabahu hii imenitendea, mume amerudi nyumbani. Alikuwa anawanyanyasa watoto, lakini sasa hivi watoto ndo amewakumbatia. Mwanaume alikuwa ni mbaya sana mpaka akawafukuza watoto ndani ya nyumba, wakazagaazagaa akashindwa kuwasomesha. Kwa kweli iliniuma sana, lakini sasa hivi mume wangu amesharudi nyumbani, namshukuru Nabii Flora, madhabahu hii inatenda, ukiamini kweli utafanikiwa, kweli mimi nimefanikiwa.


AMINA JUMA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMRUDISHA MUME WAKE NYUMBANI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Amina Juma; namshukuru Mungu wa Nabii Flora, mume wangu alikuwa ameniacha, lakini baada ya kufika hapa na kuombea, sasa hivi amerudi na alipokuwa amepeleka vitu vyake amerudisha, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa kunitendea. Napenda kuwaambia mtu yeyote anayepata mateso kwenye ndoa, aje hapa kwa Nabii Flora anaweza.

------------------------------------------------

MAHUBIRI YA TAREHE 16 01 2014
Mungu ametupigania, ametupa pumzi ya uhai, tu wazima kwaajili ya neema yake tu, tumemuona Mungu akiwa pamoja nasi katika siku hii ya leo, na leo ni siku ya nne ya Kinabii, ambayo Mungu alimvika kiatu Nabii. Nilizungumza juzi katika siku ya kwanza ya uumbaji, tuliongea katika 2Nyakati 20:26-30, nikasema siku ya nne usikosekufika katika nyumba ya Bwana. Ninazungumzia sana habari ya siku ya nne ya leo, ambayo ni siku ya Kinabii Mungu alimvika Nabii kiatu na koti.

2 Nyakati 20:26-30
Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia jangwani, nao Yehoshofati na watu wake walipokuja kuchukuwa nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali na mavazi, na johari za thamani; anasema waliona sana kati yao wingi wa mali, na katika mwaka huu kutakuwa na wingi sana wa mali, baraka, majibu, kufanikiwa. Anasema ndipo Yehoshofati na wengine wote walipokuwa wameingia katika ile nchi, kama tulivyoingia sisi katika mwaka 2014, ndipo akaona Yehoshofati Nabii wingi sana wa mali na wingi wa mavazi mazuri.

Walijichukulia zaidi kuliko wawezavyo kuchukuwa; nataka mwaka huu ujichukulie baraka, mavazi mazuri kuliko uwezavyo kuchukuwa. Mungu wetu ni mwema hakuna jambo linalomshinda Mungu, katika mwaka huu unakwenda kufanikiwa ni mwaka utiririkao maziwa na asali, nataka ufanikiwe mwana wa Mungu kwa mwaka huu. Huu ndio mwaka ambao Yehoshofati Nabii siku ya tatu, wakakusanya nyara, fedha, dhahabu kwa kiasi wasichoweza kubeba, nataka na wewe ufanikiwe, hakuna jambo linaloshindikana kwa Mungu wetu, yote kwa Mungu yanawezekana. Kila nikitazama nikipiga taswira katika ulimengu wa Roho, ninaona baraka zinakuja kama mvua, mafanikio yanakuja juu yako, ninaona ushindi unakuja juu yetu, teka nyara sasa tena usiteke vichache teka vitu vingi.

Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la baraka, maana ndipo alipowabarikia Bwana; anasema hata katika siku ya nne, na leo ni siku ya nne ndipo Mungu alimvika Nabii kiatu na koti, yaani maana ya koti ni utukufu, viatu ni mamlaka. Nataka nikuingize nikupatanishe katika siku a Kinabii, upate wewe kuingizwa katika bonde la baraka. Yaani leo ndiyo siku yako ya kubarikiwa, anasema siku ya nne, siku ya Kinabii ambayo waliita bonde la baraka, hapo ndipo Bwana, ukisikia Bwana ni Yesu, ndipo alipowabarikia. 

Ulikuwa hauzai unakwenda kuzaa, ulikuwa hauna mtoto unakwenda kupata mtoto, haijalishi watu wanapata mimba wanazitoa kesho, leo ni zamu yako tutakamata vizazi vitakuja kwako alafu wewe utapokea mtoto, pokea baraka. Leo ni siku ya wewe kuitwa bonde la baraka, ni siku yako ya kuingizwa katika bonde la baraka, nataka nikubariki wewe uliyefika hapa, nakutamkia baraka kwa jina la Yesu Kristo, nasema pokea mtoto wa kiume na wa kike. Nasema pokea kazi kwa damu ya Yesu.

UJUMBE WA NENO LA MUNGU UNATOKA KATIKA KITABU CHA KUMBUKUMBU LA TORATI 26:1….
Na itakuwa ukishaingia katika nchi akupayo Bwana, iwe urithi na kuimiliki na kukaa ndani yake; yaani uingie uimiliki hii nchi, na ukishaimiliki upate kukaa ndani yake, yaani tumeingia hapa katika nchi ambayo Mungu ametupa, tupate kumiliki yaliyomema, utajiri, na baraka zote, kisha kumiliki tukae ndani yake bila kufa.

Toa malimbuko ya ardhi utakayovuna akupayo Bwana Mungu wako, ukayatie katika kitabu, ukaweke mahali alipopachagua Bwana, ili aliketishe jina lake. Ninakiri leo mbele ya Bwana Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi aliyowaapia baba zetu; malimbuko ni sehemu ya mshahara wako, hakika umekuja hapa lazima uponywe, uponyaji, kubarikiwa ni lazima hapa, ukija hapa hufi na TB, Kansa, Pressure, nasema hutokufa unakwenda kuishi.

Naye kuhani akakipokea kikapu mikonono mwako, atakiweka chini mbele ya madhabahu ya Bwana, nawe utajibu na kusema mbele za Bwana Mungu wako. Baba yangu alikuwa Mualami, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao walikuwa ni wachache sana hesabu yao. Lakini Mungu aliwabariki, wakawa taifa kubwa kuliko wenyeji; napenda nikwmabie haijalishi wewe, umekuja hapa ukiwa mgeni, utakwenda kuwa taifa kubwa, tunakwenda kuongezeka mwaka huu, tutakuwa na utajiri kuliko wale waliokutangulia, haijalishi wewe unaonekana kama mgeni. Nami nasema tunakwenda kuwa na taifa kubwa, tutakuwa na maelfu ya watu, wamekuona wewe ni mtu wa chini unakwenda kuwekwa juu, unakwenda kuinuliwa, kupokea baraka. Haijalishi watu wamekudharau.

Wamisri walituonea, wakatutesa, wakatutumikisha katika mtumwa mzito, tukamlili Bwana Mungu wa baba zetu, Bwana akasikia sauti yetu akaona taabu yetu; anasema Bwana ameona taabu yetu, masikitiko yetu sasa ameshuka kutuingiza katika nchi ya maziwa na asali. Mwaka huu Mungu ameona mateso yako, ameshuka ili wewe akufanikishe, huu ni mwaka wako wa kutendewa.

Ameona taabu zetu na kuonewa kwetu, Bwana akatutoa katika Misri, akatuingiza mahali hapa na kutupa nchi hii, nchi ijaayo maziwa na asali; yaani Bwana anakutoa katika Misri, yaani katika mikono ya majuto, mateso, magonjwa ulionayo, unakwenda kuingizwa katika bonde la baraka, mwaka huu ni mwaka wako wa kutendewa kwako. Wapendwa Bwana ametutoa kule mwaka jana, akatingiza katika mwaka huu 2014, katika mwezi wa Nisani, tumeingizwa katika nchi iliyojaa maziwa na asali, tupate kuishi maisha ya urojourojo. Ametuingiza hapa tupate kumiliki mafanikio ya nchi hii, tumili maziwa na asali.

 --------------------------------------

JINSI YA KUFIKA KANISANI
Kama unatokea Mwenge panda magari ya Tegeta, shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni, uliza kanisa la Nabii Flora Peter

Tembelea



No comments:

Post a Comment