DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Friday, February 28, 2014

MUNGU WA MBINGUNI AZIDI KUFANYA MIUJIZA, ISHARA NA MAAJABU KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI. SHUHUDA HIZI ZA JUMAPILI 16.02.2014 ZAWEZA KUKUINUA KIIMANI


Bwana Yesu Kristo apewe sifa!!! Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya hapa kanisani kwetu. Tunasikia shuhuda nyingi sana zenye kuinua imani zetu. Watu wanazidi kutendewa maajabu na Mungu wetu wa Mbinguni.

Na hii yote ni kutokana na upendo wa Mungu kwa watu wake. Juhudi zako za kumtafuta Mungu na kuwa mwaminifu zitakufanya ujibiwe swali lako. Zidi kumtumikia Mungu na kuachana na dhamibi, kuwa mtoaji ili kazi ya Mungu izidi kukua, fanya yaliyo ya Mungu na Mungu atakubariki na kukutatulia matatizo yako. Soma shuhuda hizi


JINSI YA KUFIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASLA KWA NABII FLORA PETER
Kama unatokea Mwenge, panda magari ya Tegeta, shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisani kwa Nabii Flora peter




SHUHUDA MBALIMBALI

BABA ANAMSHUKURU MUNGU KUMPONYA MWANAYE


Bwana Yesu asifiwe; madhabahu hii ya Nabii Flora, siku moja nilikuwa kazini, ilikuwa muda wa saa kumi nikapigiwa simu mtoto wanaumwa, nikachuwa usafiri kweli nikafika mpaka Tegeta, nikakuta mtoto wangu anataka kukimbia, nikamkamata tukalala tumemshikilia mpaka asubuhi. Asubuhi ile tukachukuwa usafiri tukaja hadi Hospitali moja ipo Kibaoni, basi wakamwangalia mtoto wakamwandikia dawa, alikuwa amelala bila kula kitu chochote akatundikiwa drip. Baada ya hapo mtoto hali iliendelea kuwa nzuri kidogo tukarudi nyumbani, tukalala ilipofika saa kumi na moja mtoto akawa anasema Baba kuna watu wanataka kuniua hata baba na wewe ukiwemo. Tukamrudisha Hospitali Daktari akasema tumpeleke Muhimbili, lakini mama mmoja akasema tumlete kwa Nabii Flora. Basi tukaja hapa tukaangaika naye mpaka tukafika kwenye meza ya Nabii Flora, Nabii akasema huyu mtoto atapona wala msiwe na wasiwasi. Nilijisikia kuwa na imani kwa sababu niliangaika sana, na sasa hivi namuamini Mungu wa madhabahu hii ya Nabii Flora, naimani mwanangu amepona kabisa kwa uwezo wa mwenyezi Mungu wa Nabii Flora

DADA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MDHAMINI KWAAJILI YA KAZI YAKE YA MUZIKI WA INJILI

Bwana Yesu asifiwe; namshukuru Mwenyezi Mungu wa mahali hapa anatenda makubwa, Jumapili iliyopita nilikutana na mtumishi wa Mungu Nabii Flora, nikamweleza kuhusu matatizo yangu, nikamwambia nimechoka kuitukuza dunia.



Sasa kwa nini hii sauti nzuri iendelee kutukuza walimwengu wakati yeye aliyenipatia hii sauti nishindwe kumuinua, nahitaji sasa hivi kumtukuza ila sina uwezi, nimetengeneza sasa hivi nyimbo moja. Nabii akaniambia hii wiki haitapita utapata mfadhili, alipokuja huyo mfadhili siku ya kwanza alikuwa ananishangilia tu hakuniambia chochote, siku ya pili akaniambia dada unasauti nzuri kuanzia leo mimi nitakuwa mfadhilia wako.

Nikasema Mungu wangu ambaye anamuinua Nabii Flora mahali alipo pale Salasala wakati huu akipiga goti lake yeye kwaajili yangu mimi basi akubariki wewe kazi yako ya mikono unayofanya, huku unakokwenda urudi basi akubariki na wewe uweze kunibariki. Akaniambia naenda Iringa kununua uwanja mkubwa sana kwa sababu ya kazi zangu, nikirudi uniambie mahitaji ya studio ni shilingi ngapi ili niweze kukudhamini.

DEO DAUDI ANAMSHUKU MUNGU BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMERUDISHWA KAZINI


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Deo Daudi; nilikuja hapa nilikuwa nasumbuliwa sana na viupele katika mwili wangu, pia nilikuwa sina kazi, kwa hiyo nilipofika hapa Nabii Flora akanipa sabuni. Baada ya kuondoka hapa nilipofika nyumbani nikaogea sabuni hii, nilimsalimia mama mwenye nyumba akakataa kuitika, kumbe ni sabuni hii imeshaleta madhara katika ile nyumba. Asubuhi nilipoamka nikamsalimia tena akakataa kuitika, nikasema ngoja niendelee kuitumia hii sabuni nione nini kitatokea, ilipofika siku ya tatu, kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi lakini nilisimamishwa, bosi akanipia simu akaniambia njoo uendelee na kazi. Namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa aliyonitendea kwa sababu sikutegemea kama nitapata miujiza kama hii, na mama mwenye nyumba sasa nikimsalimia anaitika, shetani maeshindwa kwa jina la Yesu.

FLORA JUSTINE ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA MAOMBI YA NABII FLORA MDOGO WAKE ALIYEKUWA AMEKAMATWA NA MAPILOSI AMEACHILIWA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Flora Justine; nilikuja hapa mdogo wangu alishikwa akawekwa rumande, alizuiliwa hata zamana asiwekewe, mama alizunguka huku na huku lakini ilishindikana. Nikamwambia mama subiri naenda kwa Nabii Flora utasikia mdogo wangu ametoka, nilipokuja hapa akaombewa, ilipofika saa tatu mama akanipigia simu, akasema mapolisi wamempigia simu kwamba mdogo wangu ameruhusiwa kutoka. Namshukuru Mungu wa Nabii Flora mdogo wangu ametoka, alikuwa mkoa wa Musoma.


EDNA MPANZI ANAMSHUKURU MUNGU KUPATA KAZI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Edina Mpanzi; namshukuru Mungu, mimi nilipofika kwenye madhabahu hii nilikuwa sina kazi, hata nauli ya kuja hapa nilikuwa Napata kwa shida, naombaomba tu. Lakini sasa hivi ninamshukuru Mungu nimepata kazi kwenye madhabahu hii hii ya Nabii Flora.




GERALD MICHAEL ANAMSHUKURU MUNGU RAFIKI YAKE AMETOKA JELA PIA YEYE MWENYEWE AMEPATA KAZI ALIYOKUWA ANAITAKA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Gerald Michael; namshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyoyatenda, kulikuwa na rafiki yangu alikuwa amewekwa ndani na kulikuwa hakuna zamana wala kutoa rushwa. Lakini Mungu wa mahali hapa anayetenda makuu, ilikuwa mwaka jana mwezi wa 12, nikamsii Mungu, Mungu akatenda, akapata kuwa huru. Mwezi wa pili mwanzoni bado Mungu aliendelea kututenda, tulikuwa tunajenga saiti moja kwa askari mmoja, basi alitaka kufanya tena hila ili nisirudi tena kule kazini, Mungu akaziba ndani yake, niliondoka saa kumi usiku na nilipanga kuondoka saa kumi na moja. Basi namshukuru Mungu ameendelea kuonekana tena, nilienda sehemu moja kuomba kazi, nilipofika pale nikanyimwa kazi, lakini nikapata kazi moja ambayo sikuifuraia lakini nikafanya hivyo hivyo. Siku ya pili nikaenda nikawaambia kazi hiyo siifanyi nataka kazi nyingine, Mungu alitenda kitu cha ajabu sana, pale kazini walikuwa wanatoa pesa ndogo sana, lakini baada ya kufika mimi zile siku mbili mshahara ukaongezwa, na walikuwa hawajawai kununuliwa juice hata siku moja na Engineer, lakini siku hiyo walinunuliwa. Wakasema ni nini kwani una nini wewe, nikawaambia ninamwamini Mungu anayetenda, na ninatokea kwa Nabii Flora. Siku ya jana tuliambiwa na bosi tufanye kazi lakini miili yetu ilikuwa imechoka, tukasema hatufanyi kazi, kwa hiyo hatukufanya kazi, na leo nikasema naondoka kwenda Kanisani Mungu utende kazini kwa sababu nikiondoka anapewa mtu mwingine, namshukuru Mungu mvua inanyesha kazi hakuna imesimamishwa.

GLADNESS JACKSON ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER, NYUMBA WALIYOKUWA WANATAKA KUZULUMIWA IMESHINDIKANA KUZULUMIWA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Gladness Jackson; nauhakika kabisa watumishi wa Mungu pale mbele nilishawahi kuongea nao kupitia picha ya nyumba yangu, hii sticker ya Nabii Flora imefanya mambo makubwa sana kwangu ambayo miaka 4 iliyopita sikutegemea kama itatokea. Hii sticker nilinunua muda mrefu kulikuwa na kaka yangu anaumwa, na shangazi yangu alikuwa anaumwa, na sisi tulikuwa na matatizo ya nyumba, sasa nikawa najishahuri sijui niiweke kwenye picha ya nyumba yangu, sijui niiweke kwa shangazi au nimpelekee kaka yanagu.

Nilipokuwa nawaza niibandike kwenye picha ya nyumba yangu, nikawa nimeibandika chumbani kwangu, nikamwambia mume wangu tuangalie hii picha tumuombe Mungu hii nyumba itakuwa ya kwetu. Sasa Ijumaa nikawa nimeenda kazini, niliporudi mume wangu akaniuliza Jumatatu unaenda kazini, nikamwambia ndio kwani kuna sikukuu yoyote, akaniambia hapana hakuna sikukuu, nikamwambia kwani kuna nini, akaniambia ngoja kwanza tule alafu nitakwambia kuna kitu gani kimetokea. Kwenye hii nyumba madalali wameshapelekwa nyumba inauzwa milioni 80, wakati sisi tulinunua kiwanja milioni 1 na tukajenga hii nyumba mpaka hapa tulipofikia. Basi tulipokuwa chumbani nikawa sina amani, nikamwambia mume wangu kwani kuna nini, akaniambia tusalikwanza maana hatujasali. Ilikuwa juzi Ijumaa nilikuwa fellowship mchungaji akanipigia simu akaniambia njoo officen kwangu, alipoenda akamkuta Yule mchungaji ambaye lile eneo tulilinunua kwake, tukawa tumeelewana tulipe milioni 25 ili kufidia kile kiwanja ndugu yake kutoka Arusha amekuja yupo pale kwa mchungaji. Yule baba akasema kwa kweli hii imeshakuwa ni laana katika ukoo wetu, hatutapenda kitu kama hiki kitokee wala hatutaweza kujenga wala kuishi kwenye nyumba hii, akasema kesho Jumatatu tutakuja hapa officen Mr. Kimaro utakuja na mke wako na nyie wengine mtakuja tukutane hapa, tunataka hili tatizo liishe kuna kiwanja kipo Tabata Segerea tutaenda kukiangalia, tutapatana na Yule mtu mtanunua mumfidie Yule mchungaji kile kiwanja, ambacho Yule mchungaji tulikabidhi milioni 15 na risiti tunazo. Kwa hiyo Mungu wa Nabii Flora ameenda kutenda miaka 4 ambayo tuliishi kwa mateso.


HAPPINESS ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI
HAPPINESS ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Happiness; namshukuru Mungu nilikuja hapa ninawashwa, Nabii aliniambia nilete maji akayaombea. Yale maji nikayaogea, na nikayanawia huku chini, yaani nilijiona kama naota mpaka sasa hivi siwashwitena, sasa hivi nimepona kabisa namshukuru Mungu, pia napenda kuwaambia watu wote tumwamini Mungu.




HENDREW ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA NA SASA AMEPATA KAZI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Hendrew; niliangaika tangu mwezi wa tisa sina kazi, nilijaribu kuangaika makampuni yote na bahasaha yangu kama chizi. Juzi nikaitwa nikafanye interview nikafeli, nikaitwa tena kwenye interview nyingine nikafahulu lakini jina halionekani, ndo nikaja hapa kwa Nabii Flora nikamwambia mimi nimepata interview, vyeti vyangu hivi hapa na lessen na maji haya hapa naomba unibariki. Kwa kweli nilivyotoka hapa saa 7 nikawa mtu wa 7 kufahulu, nilikuwa na test nne ya kwanza nikapata mia, na ya pili nikapa mia kwa hiyo kesho nakwenda kusaini mkataba, namshukuru sana Mungu.
JASMINI ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA VIRUS VYA UKIMWI BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Jasmini John naishi Manzese; kwa kweli madhabahu hii ni ya hatari na inatisha, napenda kuwaambia muamini na kukubali Mwenyezi Mungu atawajalia, watoto wangu wadogo nimewazaa katika mazingira ya HIV. Lakini juzi kwa uwezo wa madhabahu hii, nampenda Nabii Flora kwaajili ya sabuni hii, Jumapili hadi Jumatano kwenda kupima nikakuta Negative. Nilikuwa na Virusi vya UKIMWI na watoto wangu toka mwaka 2009 mpaka 2014, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa kuniponya.
JULIUS ANAMSHUKURU MUNGU KUMWEZESHA KUAPA FEDHA ALIZOKUWA ANAZIITAJI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Julius; tarehe 27 mwezi uliopita kuna kazi ilikuwa ifanyike inaitaji shilingi milioni nane, lakini nikakosa kabisa zile pesa, nikampigia mama mchungaji Ansila nikamwambia nahitaji shilingi milioni 6, akapeleka simu kwa Nabii, nikamwambia

Nabii mimi nataka pesa shilingi milioni 6, Nabii akaniambia nakuombea upate hizo pesa. Siku ya Alhamisi nikakuta mtu ameniletea milioni 4, Ijumaa mwingine akaleta milioni 4 kwa hiyo zikawa milioni 8, kwa kweli nilishukuru sana nimepata milioni 8 badala ya milioni 6, kwa kweli mama amenisaidia sana.

KAKA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPA KIBALI KATIKA MKUTANO
Bwana Yesu asifiwe; toka nimekuja hapa na kuogea sabuni na maji, nilikuwa na mkutano nashukuru Mungu nilizungumza virusi, haikuwa mimi bali ni kwa neema ya Mungu tu, kiwango cha shule mimi ni darasa la saba. Mpaka kufikia jana nilikuwa naongea na muasibu wa ubalozi wa Marekani kupitia biashara zangu. Kwa kweli napenda kusema Mungu wa madhabahu hii anatenda, Mungu aendelee kumbariki Nabii Flora, aendelee kuliinua taifa la Tanzania hata sisi vijana tuweze kuonekana katika taifa letu. Asante sana mama nakuombea kwa Mwenyezi Mungu, Mungu akubariki kwa sababu Mungu anaamini watu wake wanafanya mambo ya ajabu katika ulimwengu.
LUCY ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER AMEMUEPUSHA NA KIJANA ALIYEKUWA ANATUMIA NJIA ZA GIZA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Lucy; Mungu amenitendea mambo ya ajabu sana kupitia madhabahu hii, ilikuwa wiki iliyopita siku ya Ijumaa nilikuja katika madhabahu hii, nilipotoka hapa nilikutana na kaka mmoja njiani akaniambia anaomba uchumba kwangu, lakini nikamwambia mimi sijisikii sasa hivi kuwa na mtu. Akaniambia naomba nije kwako, nikamruhusu, alipofika kwangu pindi naongea naye nikamuona anabadilika sura, sasa nilikuwa na hofu jinsi ya kumsaidia nikakemea, nikachuwa hii sticker nikamwekea, akaniuliza wewe una Mungu wa aina gani shetani ametoka, nikamwambia mimi ninamuamini Mungu wa Nabii Flora. Nikaja kwa Nabii Flora nikamwelezea akaniambia huyo ni jini, lakini mimi nilikuwa na hofu, nikachukuwa sabuni hii iliyoombewa na Nabii Flora nikaogea. Baadae ile hofu ikawa imeondoka, akanipigia simu nikamwambia njoo nyumbani, nikachukuwa hii sticker nikaibandika ukutani, na hii sabuni nikatengeneza povu nikamwaga mle ndani. Nilipofanya hivyo akaniambia mimi huko sitakuja najisikia vibaya, nikazidi kumwambia Mungu wa Nabii Flora aendelee kutenda kupitia sticker hii irihirike huyu kijana anataka nini. Baadae tena akanipigia simu nikamsisitiza kwamba naomba njoo, akaniambia mimi nakuja niandalie chakula, kweli nikamwandalia chakula lakini akaniambia tena sitafika huku.
LUCY ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER AMEMUEPUSHA NA KIJANA ALIYEKUWA ANATUMIA NJIA ZA GIZA

Akapiga tena simu akaniambia nakuja, nikamwambia karibu, alipokuja nikaenda kumpokea alikuwa na chupa ya maji, akaniambia nimekulea maji ni zawadi yako, nikamwambia asante, akanikabidhi yale maji nikamwambia shindwa kwa jina la Yesu. Basi nikamwandalia chakula, chaajabu sehemu niliyokuwa nimebandika sticker ghafla nikaikosa ile sticker, nikasema Mungu wa Nabii Flora kwa nini nataka kushindwa, lakini nikasema hapana Mungu wa Nabii Flora hawezi kushindwa. Nikamtengea chakula nikabariki kile chakula kwa kupitia Mungu wa Nabii Flora, akasema basi mimi sitakula hiki chakula, nikamwambia naomba ule kuwa na amani, akawa anakula lakini hana amani. Nikamwambia mbona nakuona hauna amani, akaniambia najisikia kizunguzungu, basi baada ya kumaliza kula nikampa hiki kipande cha sabuni anawie. Aliposhika hii sabuni akaniambia mbona najisikia kizunguzungu, nikamwambia kwa nini, akaniambia mimi mwenyewe sielewi kwanza mimi nakuogopa, nikamwambia unaniogopa mimi jini. Basi baada ya hapo akaniambia mimi naondoka, nikamwambia siulikuja kwangu nieleze ulichofuata, akasema hapana mimi naondoka akachukuwa simu akawa anampigia mtu wa bodabda aje amchukuwe. Basi mwenye pikipiki sijui kama alikuja lakini aliniambia nifungulie mlango mimi niondoke, nikamwambia haya akatoka, kafika njiani akanitumia meseji akaniambia dada kuanzia leo sitaki unipigie simu wala mimi sitakupigia simu. Kweli Mungu wa Nabii Flora anatenda miujiza, ukiamini kweli utapata, na usipo amini utateseka.

MAMA MCHAKI ANAMSHUKURU MUNGU MWANANE BAADA YA KUTUMIA STICKER AMEWEZA KUPATA KAZI YENYE MSHAHARA MZURI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mama Mchaki; namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa mambo aliyonitendea kuhusu sticker na sabuni, kulikuwa na mtoto wangu alipata kazi bila kufanya interview. Hii sticker ni ushuhuda mkubwa sana kwangu, nilimnunulia nikasema kwa sababu wewe hupati nafasi ya kuja Kanisani kwa Nabii Flora, naomba niwe napeleka maombi yangu mbele, nasali hapa kwaajili ya mtoto wangu. Lakini mwenyezi Mungu alivyonitendea siku ya Jumatano jioni, muda wa saa kumi na mbili alipata simu kwamba anaitajika kwenda kufanya interview.
Alipokwenda kwenye interview nikamwambia hii sticker utakwenda nayo, utakapokuwa unafanya interview utajiambatanisha na Nabii Flora, kweli akasema mimi nilipokuwa nafanya interview nilijiambatanisha na Nabii Flora, na sabuni niliogea, na maji niliogea na kuyanywa, nikamwambia usichoke. Alienda siku ya Alhamisi kufanya interview, kufika saa tatu wakampigia simu kwamba umepata kazi, na ambayo namshukuru mwenyezi Mungu, kule alipokuwa mara ya kwanza walikuwa wanamlipa mshahara mdogo sana, lakini sasa hivi alipokwenda wamemzidishiwa mara tatu. Kupitia sticker hii, napenda kuwaambia Watanzania wote mje hapa kwa Nabii Flora, Mungu wa Nabii Flora anatenda kila kitu unachokiomba.

MCHUNGAJI NERIKA NGOWI AMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER MWANAE AMEWEZA KWENDA KAZINI MAPEMA NA ILE HALI YA KUCHELEWA KUAMKA NA KUCHELEWA KAZINI IMEKWISHA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mchungaji Nerika Ngowi; natokea katika Kanisa lingine Kijitonyama, nilikuja kwa matumishi wa Mungu Nabii Flora kama wiki mbili zilizopita akaniombea huduma yangu. Kwa hiyo nikapata eneo la Kanisa kule Mbagala, sasa watu wakaanza kuwa wengi, watoto wamekuwa wengi, Waislamu wakaanza kunigeukia, wakaniambia mama hatukutaki hapa, wachungaji wenzangu wakachomewa makanisa, na langu likachomwa. Nikarudi Kijitonyama, basi nikapata tena eneo pale Kijitonyama. Wachungaji kama wawili walishafanya hapo huduma yule babu akawafukuza, kwa hiyo mimi nilikuwa ni mchungaji wa tatu, sasa Yule babu akaanza tena kunisumbua sumbua, nikasema sasa Mungu mimi hapa naenda tena wapi.
Nikamka saa 7 usiku nikaomba, sauti ya Mungu ikaniambia uende kwa mtumishi wako Nabii Flora, sasa nikajiuliza Nabii Flora nitampata wapi wakati Mbezi alishahama, basi nikapata mtu mmoja akaniongoza nikafika mpaka hapa. Nilipofika hapa nikachukuwa sticker nikaenda nayo nyumbani kwa imani, kwanza kabisa nilidumbukiza kwenye ndoo ya maji ya kuoga mara 7, nikasema nataka nimuone Mungu aliyemleta Nabii Flora Tanzania ili mimi nipone na wote watakaoamini, nikayaogea yale maji kwa imani kabisa. Nikaondoka nikaenda Kanisani nikamkuta Yule babu mahali pale, akaniambia mama huduma yako sasa imefika mwisho nataka nianze huduma yangu mwenyewe ya chuo cha Biblia, nikamwambia hakuna tatizo baba mimi mwenyewe ni mwalimu wa chuo cha Biblia hata ukitaka kuniajiri sawa tu. Basi tukaongea pale tukamaliza, tukafanya ibada tukatoka nikarudi nyumbani, sasa nikashika tena hii sticker usiku kama saa 7 hivi, nikanyanyua juu nikasema Mungu wa Nabii Flora shuka, uonekane pele kwenye lile eneo langu ama la Yule babu, baada ya kusema hivyo nikatulia. Siku ya kwanza, ya pili, siku ya tatu Yule babu kafa, wakaniita tukaenda tukamzika, baada ya siku mbili watu wakasema lile eneo ni la serikali za mitaa kwa hiyo tutahakikisha Yule mchungaji hana eneo. Niliposikia maneno hayo ndio nikaja tena huku kwa mtumishi nikamweleza, nikamwomba aniombee tena, akaniombea, akaniambia la muhimu sana kesho usikose lazima uje hapa utoe huo ushuhuda. Ushuhuda mwingine kuhusu hii sticker nilikuwa na mtoto ambaye usiku alikuwa alali ni kuangalia TV mpaka asubuhi. Saa nyingine anamwamsha mke wake na mtoto amakeni mnisaidie, saa ile ya kuamka asubuhi watu wanaenda kazini yeye ndo anaingia kitandani analala, hata ukimwamsha mcha ale chakula yaani ni kwa utata sana. Basi nikachukuwa hii sticker nikampa mkamwana nikamwabia ingiza kwenye mto wake anaolalia, kesho yake asubuhi mtoto mdogo wa miaka miwili akatoa ile sticker kwenye mto baba akaiona, akauliza ni nini hii mimi nalalia, mke wake akamwambia hii hapa ni sticker mama alileta ulalie ili uweze kupona. Siku ya pili akalalia, sikua ya tatu akaamka saa kumi na moja akajiandaa kwenda kazini.

MONIKA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMUEPUSHA NA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MOROGORO BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA, PIA MBWA NA PAKA WALIOKUWA NYUMBANI KWAKE WAMEONDOKA 

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Monika; madhabahu hii imenitendea mambo makuu sana, nilikuja hapa kama wiki tatu zilizopita, nilikuwa na msiba nikaenda kwa Mchungaji Ansila, nikamwambia nataka kusafiri naomba nimuone Nabii ili aniombee. Nikaonana na Nabii akaniombea ile safari, nikasafiri nilikuwa mimi na mdogo wangu, sisi tulishuka Ipogoro, wenzetu walioendelea mbele baada ya masaa mawili walipata ajali. 
Tulikuwa tunawapigia simu ili kuwajulia hali lakini simu zilikuwa hazipatikani, na baada ya hapo tukakaa wiki mbili bila mawasiliano, kwenye lile gari mmoja alinusurika akawa amelazwa hospitali. Alimpigia simu mdogo wangu akamwambia msalimie Monika, mwambie kwenye lile gari tulipata ajali na mimi ndio nienusurika peke yangu na sasa hivi nipo Hospitalini nimelazwa. 
Kwa hiyo namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora, kwa sababu lile gari tulikuwa twende mapaka Morogoro, lakini nilikuwa na sticker na kila ajali ilipokuwa ikitaka kutokea nikamwambia Mungu wa Nabii Flora naomba utuokoe, gari letu likafunga breki na kulikuwa na roli kubwa nalo nikafunga breki. Sisi tulishuka saa tisa na lile gari lilifika saa kumi na moja, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora. Pia kwenye nyumba yangu kulikuwa na mapaka yanalia kama watoto, na mbwa wanacheza barazani, lakini toka nimeanza kusali katika madhabahu hii, sijaona tena mbwa wala paka. Ila majirani wote wakawa wamenisusia, namshukuru Mungu sana.


PILI MOHAMED ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA MWANAE BAADA YA KUTUMIA MAJI YALIYOOMBEWA NA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Pili Mohamed; mimi nilikuwa mtu wa shetani, lakini baada ya kufika hapa kwa Nabii Flora, nimepata kuinuka na kulijua neno la Mungu. Pia nyumbani kwangu wanangu walikuwa hawaishi kuumwa, kama Jumapili iliyopita mwanangu alikuwa anaumwa sana, mume wangu akaniambia tumpeleke kwa mganga, mimi nikamwambia siwezi kwenda nina Mungu wa Nabii Flora nitamtumia. 
Nikachukuwa maji nikamuogesha mwanangu na kumnywesha, sahiyo hiyo akatapika akapata fahamu, nikamwambia mwanangu kinachokuuma ni nini, akaniambia nilipita njia panda nikaokota mia hamsini, nilivyoitumia nilijisikia kizunguzungu nikadondoka.
Akaniambia mahali hapa nilipofikia namshukuru Mungu wa Nabii Flora na Kanisani twende wote, na mwanangu nipo naye hapa hapa Kanisani, nashukuru sana haya maji yamenitendea sana.
SAMSON MASANJA ANAMSHUKURU MUNGU ALIKUWA AMESIMAMISHWA KAZI LAKINI BAADA YA KUOGEA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMEAMBIWA AKAENDELEE NA KAZI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Samson Masanja; Mungu wa mahali hapa amenitendea, toka nilipoogea ile sabuni, nilipokuwa nafanya kazi nilikatishwa mkataba, ilipofika jana nilipigiwa simu nikaendelee na mkataba wangu, namshukuru sana Mungu.

SARA MPINGA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA MWANAE VIUPELE MWILINI BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Sara Mpinga; madhabahu hii ya Nabii Flora imenitendea kuhusu mtoto, huyu mtoto wakati anarudi shule aliniambia kwamba ameokota pesa shilingi mia tatu katika uwanja wa mpira.
Lakini nilisema labda ni watoto wamedondosha kwa hiyo hakuna neno, lakini siku ya pili alitokwa na vipele mwili mzima, wakati huo nilikuwa nimeshachukuwa sabuni iliyoombewa na Nabii Flora. Nikamwambia ngoja nitatumia hii sabuni niliyotoka nayo kwa Nabii Flora itakusaidia mwanangu, akaniambia sawa mama. SARA MPINGA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA MWANAE VIUPELE MWILINI BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA

Nikamuogesha siku ya kwanza, ya pili na ya tatu, kuja kumwangalia nikakuta vile vipele vyote hakuna, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora. Napenda kuwaambia wenzangu tuwe waaminifu na kuelewa yale maneno anayoongea Nabii Flora, nilikuja kwa mambo mengine lakini Mungu kanitendea hili, naimani hata mwanangu aliyekufa katika mazingira ya kutatanisha atarudi.

STELLA MBINSI ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA SEHEMU YA KUISHI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Stella Mbinsi; namshukuru Mungu nimepata mahali pa kuishi, nilikuwa nalala hapa Kanisani, kesho nitaondoka kwa hiyo namshukuru Mungu
You might also like:

No comments:

Post a Comment