DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Friday, February 28, 2014

JAMANI NISAIDIENI, MUNGU ANASEMA NINI JUU YA USHOGA? WALE MASHOGA MAARUFU SANA NCHINI MALAWI WAPIGANA VIBUTI,NA KUWA GUMZO KILA KONA:


Kabla hujaendelea kusoma huu mkasa wa hawa mashoga, nataka kwanza unijibu kuhusiana na Biblia au Neno la Mungu linasemaje  juu ya ushoga? Wewe kama msomaji wa Biblia utajua nini Mungu wa mbinguni anasema juu ya hii tabia ya kuoana wenyewe kwa wenyewe. Mimi sina comment ila ninavyojua ni kwamba vitabu vitakatifu vimekataza hali ya ushoga...

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga

SASA ENDELEA KUONA WATU WANAVYOFANYA HAPA DUNIANI


Tiwonge Chimbalanga (kulia) na Steven Monjeza WIKI moja baada ya mwanamuziki wa kike wa Marekani kufanikisha kuachiliwa huru kutoka gerezani kwa mashoga wawili wa Malawi ambao walikamatwa na kuhukumiwa kwa kufanya ushoga, Steven Monjeza amemwacha Tiwonge Chimbalanga na kwenda kuoa mwanamke.

Steven aliviambia vyombo vya habari kwamba alikuwa amechoka na uhasama uliokuwa unamkabili si kutoka katika jamii tu, bali kutoka kwa familia yake pia na ameamua kuachana kabisa na ushoga.

"Nimechoka. Nililazimishwa kuingia katika ufuska huo na ninajuta. Nataka kuishi maisha ya kawaida... si maisha ambayo kila mtu atanitazama, kunicheka na kunizomea."


...Steven Monjeza (kushoto) akiwa na Tiwonge Chimbalanga Hivi sasa ameanza uhusiano na msichana mwenye umri wa miaka 24 kutoka mjini Blantyre. Na Tiwonge bado ana msimamo wa kumpenda Steven, akisema kwamba mwenza wake huyo wa zamani ameamua kuchukua mwanamke kwa ajili ya "kumuumiza roho".

Aliongeza kusema: "Lakini sina wasiwasi. Huwezi kulazimisha penzi, kwani hakuna mtu aliyemlazimisha tulipofunga ndoa yetu ya kihistoria mwezi Desemba.... Bado nitaolewa kwani kuna wanaume wengi wazuri. Nitaendelea kuwa shoga."

Bonyeza hapa kujua habari ilikotoka

No comments:

Post a Comment