DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Monday, March 17, 2014

SHUHUDA MBALIMBALI KANISANI KWA NABII FLORA ZA INUA IMANI ZA WALIO WENGI..WAWEZA KUWA MMOJAWAPO


SHUHUDA ZA 02/03/2014

VIVIAN ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA MAJI NA SABUNI VILIVYOOMBEWA NA NABII FLORA AMEWEZA KUFAHULU ZOEZO WALILOPEWA KWAAJILI YA KUPIMWA AKILI ZAO, DARASA ZIMA YEYE PEKE TAKE NDIYE ALIYEFANYA VIZURI



Bwana Yesu asifiwe, naitwa Vivian; mimi nipo darasa la tano na mimi peke yangu ndiye mwanafunzi ambaye nimeamia katika ile shule darasa la tano, siku ambayo mwalimu aliingia darasani alitupa zoezi ambalo alikuwa anatupima akili zetu. Kwa sababu nilikuwa nimebeba maji ambayo yalikuwa yameombewa na Nabii Flora, mwalimu alikuwa akiingia darasani akisema anatoa test nilikuwa nachukuwa daftari la test nageuza kule nyuma nanyunyuzia yale maji ya Baraka. Na siku hiyo ambayo mwalimu alitugaiya hilo zoezi lilikuwa ni swali moja, nikasema mimi sasa nitafanyaje swali lenyewe silijui. Nikachukuwa hii sabuni nikalamba, nikachukuwa na daftari langu ambalo nafanyia mahesabu nikapitia mahesabu ambayo tulishafundishwa, nikasema sasa nimeshapata ufahamu. Nikaandika mara ya kwanza nikana nimekosea nikakata, nikaandika mara ya pili nikasema hapa naenda kupatia, nikampelekea mwalimu anisahishie mwalimu akasema subiri mpaka wenzako wamalize kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kumaliza. Tulipokusanya madaftari mwalimu aliposahisha, akaja akasema Vivian wewe ndo umefanya vizuri kuliko wote, namshukuru sana Mungu.

SOPHIA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA SABUNI NA STICKER YA NABII FLORA AMEWEZA KUPONA MGONGO PIA ALING’ATWA NA MBWA LAKINI BAADA YA KUPAKA SABUNI NA KUBANDIKA STICKER MAUMIVU YAKAISHA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Sophia; Mungu wa mdhabahu hii amenitendea, nilikuwa naumwa mgongo miaka mingi sana, baada ya kuogea hii sabuni na kupaka sabuni mgongo umepona. Alafu juzi niling’atwa na mbwa kwenye mguu, alikuwa anaumwa sana huyo mbwa lakini baada ya kupaka hii sabuni na kubandika hii sticker maumivu yote yakaisha. Niliambiwa niende Hospitali Magomeni au nikate pale aliponing’ata, namshukuru sana Mungu kwa kuniponya.

MATRIDA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUFIKA KWA NABII FLORA NA KUOMBEWA AKAPATA KAZI BAADA YA KUTAFUTA KWA MUDA MREFU


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Matrida; namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora, toka nimemaliza chuo nilikuwa nasoma Mlimani, nilimaliza mwaka 2011, niliandika barua nyingi sana za kuomba kazi, sijawai kupigia simu hata barua moja mpaka nikawa nimekata tamaa na nikasahau kama nilisoma. Nikaja nikamuona Nabii Flora, Nabii akaniombea akaniambia unapata kazi, nilipewa siku 21 lakini ilipofika siku ya 11 nikapigiwa simu nikaambiwa natakiwa kwenda kufanya interview Tanesco, namshukuru sana Mungu wa mahali hapa.

EDWARD ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA MAOMBI, MDOGO WAKE AMEPONA NA BAADA YA KUTUMIA SABUNI AMEPATA KAZI



Bwana Yesu asifiwe, naitwa Edward Michaeli; namshukuru Mungu wa madhabahu hii Mungu wa Nabii Flora, kwanza namshukuru amemponya mdogo wangu sasa anaendelea vizuri, alinipigia simu akasema anaumwa miguu na mikono. Nikamsihi Mungu aende kutenda, amenipigia simu akaniambia anaendelea vizuri, Mungu wa Nabii Flora anatenda mambo ya ajabu. Pia mimi nilikuwa natafuta kazi, kila nikienda naambiwa katafute sehemu nyingine, nikiwa barabarani nikashangaa gari inasimama naitwa, nilipoitwa nikaambiwa kuna kazi nyumbani kwangu naitaji mafundi twende ukafanye. Napenda kuwaambia endeleeni kutumia hizi sabuni, mimi nilichokifanya nililoweka hii sabuni nikaichanganya na mafuta ya kujipata, nikishaoga nakuja napaka mafuta alafu natembea na upako wa Nabii.

ANNA MVUNGI ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMEWEZA KUPIGIWA SIMU NA MCHUMBA WAKE ALIYEKUWA AMEMUACHA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Anna Mvungi; kupitia sabuni hii niliichukuwa siku ya Jumapili, Nabii alisema atakaye chukuwa sabuni hii kama umeachwa na mchumba wake atakurudia. Baada ya kutumia hii sabuni jana wakati nakuja huku akanipigia simu akaniambia niende nikachukuwe pesa, namshukuru sana Mungu.

WILSON MSEKENA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA NYUMBA YAKE HAIJAUZWA TENA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Wilson Msekena; namshukuru Mungu kwa aliyonitendea kupitia madhabahu hii, kwa kweli mimi nilikuwa nyumba yangu nimeshaipotea, watu wa bank walikuwa wanataka kuiuza. Kuna mtu nilimzamini ili aweze kwenda kuomba mkopo, sasa Yule bwana akashindwa kurejesha marejesho bank, kwa hiyo watu wa bank mwaka jana 2013 waliniletea barua kwamba nyumba yangu wanahitaji kuiuza kwa sababu mtu wangu ameshindwa kurejesha marejesho. Nilivyokuja hapa kwa muheshimiwa Nabii Flora, nilimwambia kwamba nyumba yangu inataka kuuzwa kwa hiyo aniombee ili nyumba isiweze kupotea. Kweli Nbii Flora kwa kupitia madhabahu hii aliweza kuniombea akaniambia nyumba yako haitauzwa, nilirudi kwa imani maana mke wangu alishakataa kabisa kufanya usafi kwasababu nyumba inauzwa. Nikamwambia uwe na imani Mungu wa Nabii Flora anatenda, toka mwaka 2013.01. 16 hadi leo hii mwaka 02.03.2014, Yule Bwana amesharudisha mkopo wake, kwa hiyo Mungu wa madhabahu hii anatenda kweli, kwa hiyo naomba tuwe na imani na Kanisa hili.

WINFRIDA TADEI ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMEWEZA KUPONA MAPEPO NA MATETEKUWANGA PIA ALIKUWA HAWEZI KULA CHAKULA LAKINI BAADA YA KULAMBA SABUNI SASA ANAWEZA KULA



Bwana Yesu asifiwe, naitwa Winfrida Tadei; madhabahu hii imenitendea mambo mengi sana, mara ya kwanza nilikuwa naumwa sijielewi, nililala hapa siku tatu nakaa yaani sielewi kitu chochote, nikaonana na Nabii nilikuwa na bibi yangu, namshukuru Mungu baada ya kuonana naye nimeweza kupona. Yaani nilikuwa kama chizi sijielewi, lakini baada tu ya kuonana na Nabii Flora nimepata uponyaji, namshukuru sana Mungu. Shuhuda mwingine kupitia sabuni nilikuwa naumwa matetekuwanga mwili mzima, baada ya kuchukuwa sabuni hii nimeweza kupona na matetekuwanga yametoka. Na nilikuwa nikila chakula hapa kooni kuna viupele, nikalamba sabuni baada ya kulamba sasa hivi ninaweza kula, namshukuru sana Mungu wa mahali hapa, naamini na hizi alama wiki moja tu zitaisha.

------------------------------------------------------------------------------------------------------------
SHUHUDA ZA 28/02/2014

DADA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER NA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMEWEZA KUPATA NYUMBA NA KIWANJA


Bwana Yesu asifiwe; baada ya kutumia sabuni iliyoombewa na Nabii Flora pamoja na sticker ya Nabii Flora , nimeweza kupata kiwanja na nyumba. Namshukuru sana Mungu na sasa hivi namuomba Mungu anijalie mume.

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------
SHUHUDA ZA 23/02/2014

REGINA ANAMSHUKURU MUNGU MAMA YAKE AMEPONA UVIMBE TUMBONI BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA PIA YEYE MATATIZO YAKE YAMEISHA NA AMEPATA MCHUMBA MZUNGU


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Regina; nilikuja hapa kanisani nilikuwa na mama yangu alikuwa na uvimbe tumboni, akatumia sabuni akapona. Na mimi mwenyewe nilikuwa na matatizo yameisha, na nimepata mchumba mzungu ameniambia nijiandae mwezi wa tano nimpeleke nyumbani, namshukuru sana Mungu wa madhabahu hii.

MAMA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUFIKA HAPA NA KUOMBEWA AMEWEZA KUPATA TAARIFA ZA MUME WAKE ALIYEKUFA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA PIA ALIKUWA NA KIDONDA KICHWANI CHA MUDA MREFU BAADA YA KUPATA MAFUTA MATAKATIFU VIPANDE VYA CHUPA VIMETOKA


Bwana Yesu asifiwe; siku ya Ijumaa nilikuja hapa, Nabii akaniambia kwamba mume wangu yupo kwenye jalala la temeke, nikaenda siku ya Jumamosi nikarudi hapa siku ya jumatatu nikamwambia sijamuona. Basi Nabii akaniambia chukuwa picha nenda nayo, nikachukuwa picha nikaenda nilivyouliza baba mmoja akasema, nimemuona huyu mtu hapo amezungukwa na watu ananywele ndefu ni mchafu. Mume wangu alikufa katika mazingira ya kutatanisha, kwa kweli nilishangaa sana madhabahu hii inavyotenda. Na nilikuja hapa Jumapili Nabii akasema njooni watu wote mpake mafuta, mimi nilikuwa nimekaa nyuma binti mmoja akaja akachukuwa yale mafuta akanipa kwenye mkono, nikachukuwa yale mafuta nikapaka kichwani kwenye kidonda ambacho kina muda mrefu akiponi, nikasema Mungu kama umemtendea Mchungaji Ansila basi nitendewe na mimi. Ijumaa nachana nywele niende kwenye shughuli zangu nikaona kitu kama gamba kumbe ni kipande cha chupa, nikaja nacho mpaka hapa nikamuonyesha Nabii, Nabii akasema nakuombea aliponiombea. Nilipotoka hapa nikaenda nyumbani , nilipofika nyumbani nikasema mbona kama nasikia kingine, mtoto akaniambi kipo akatoa tena kama kilekile. Mungu wa madhabahu hii ananitendea vitu vya ajabu sana, nimetelekezwa na ndugu wa mume, ndugu zangu wenyewe hawanijali lakini nakula, Napata nauli kila kitu namshangaa sana Mungu, na hata mkiniona napendeza ni kwaajili ya madhabahu hii sina sehemu nyingine ninayotegemea. Kwa kweli mtumainie Mungu wa mahali hapa, mshikeni sana msichoke.

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------
SHUHUDA ZA 20/02/2014

MARIA EMMANUEL ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA MAPEPO BAADA YA KUTUMIA SABUNI NA STICKER NA YA NABII FLORA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Maria Emmanuel; nilikuja hapa nikiwa na umwa yaani nilikuwa hoi kabisa, nilikuwa na mapepo Nabii aliniambia yalikuwa elfu kumi, sasa nikawa siwezi kufanya kitu chochote, yaani hata kula nilikuwa siwezi mpaka nyumbani kwangu nikahama, biashara zangu nikafunga. Lakini toka nimekuja hapa kwa Nabii Flora naona mabadiliko kila siku, na mpaka sasa hivi nimepona kabisa, namshukuru sana Mungu baada ya kutumia sabuni na sticker ya Nabii Flora. Nilikuwa nikiumwa nabandika sticker, na nikioga naweka maji ya Baraka naoga, na sabuni napaka nalala nayo, mpaka leo naweza kushuhudia na ninacheka, kwa kweli namshukuru sana Mungu.

MONICA ANAMSHURU MUNGU KWA KUPATANISHWA NA MUME WAKE, PIA AMEMUOKOA NA AJALI NA BIBI YAKE AMEPONA KIDONDA KUPITIA STICKER YA NABII FLORA NA SABUNI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Monica; natoa shuhuda kupitia sticker na hizi sabuni za Nabii Flora, kuhusu sabuni, mimi mume wangu alikuwa akiniona nakuja anageukia pembeni, lakini toka nimeogea hii sabuni sasa hivi hata akiniona ananiangali, hata kusimama anasimama na mimi. Kuhusu sticker, nilikuwa nimesafiri nikaja kumuaga Nabii, Nabii akaniombea, tulivyofika Morogoro gari yetu tuliyokuwa tumepanda mbele yetu kulikuwa na lori linakuja. Lile gari lilikuwa na mwendo wa kasi na la kwetu lilikuwa na mwendo wa kasi, tulikuwa tunataka kupata ajali nikatamka Mungu wa Nabii Flora naomba utusaidie, kweli lile gari lilifunga break ghafla. Muujiza wa pili nilipofika nyumbani nilimkuta bibi yangu anumwa na kidonda kinamwasha, na kinatoa maji yaani kikianza kutoa maji kama vile kuna kimfyejeji, nikawa namuosha alafu naweka hii sticker naanza kusali huku nikitamka maneno haya; Mungu wa Nabii Flora naomba umponye bibi yangu hiki kidonda kwa sababu alikuwa anapata shida, nikamwambia bibi amini mimi nipo mpaka Jumapili, mpaka naondoka naomba Mungu wa Nabii Flora hiki kidonda kiwe kimeshafunga. Ilikuwa ni Jumamosi nikaosha kile kidonda nikaweka hii sticker, Jumapili tena nikafanya hivyo hivyo, kweli kidonda kikafunga mpaka sasa bibi ananiambia kweli mwanangu unamjua Mungu wa kweli.

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------
SHUHUDA ZA 16/02/2014

GLADNESS JACKSON ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER, NYUMBA WALIYOKUWA WANATAKA KUZULUMIWA IMESHINDIKANA KUZULUMIWA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Gladness Jackson; nauhakika kabisa watumishi wa Mungu pale mbele nilishawahi kuongea nao kupitia picha ya nyumba yangu, hii sticker ya Nabii Flora imefanya mambo makubwa sana kwangu ambayo miaka 4 iliyopita sikutegemea kama itatokea. Hii sticker nilinunua muda mrefu kulikuwa na kaka yangu anaumwa, na shangazi yangu alikuwa anaumwa, na sisi tulikuwa na matatizo ya nyumba, sasa nikawa najishahuri sijui niiweke kwenye picha ya nyumba yangu, sijui niiweke kwa shangazi au nimpelekee kaka yanagu. Nilipokuwa nawaza niibandike kwenye picha ya nyumba yangu, nikawa nimeibandika chumbani kwangu, nikamwambia mume wangu tuangalie hii picha tumuombe Mungu hii nyumba itakuwa ya kwetu. Sasa Ijumaa nikawa nimeenda kazini, niliporudi mume wangu akaniuliza Jumatatu unaenda kazini, nikamwambia ndio kwani kuna sikukuu yoyote, akaniambia hapana hakuna sikukuu, nikamwambia kwani kuna nini, akaniambia ngoja kwanza tule alafu nitakwambia kuna kitu gani kimetokea. Kwenye hii nyumba madalali wameshapelekwa nyumba inauzwa milioni 80, wakati sisi tulinunua kiwanja milioni 1 na tukajenga hii nyumba mpaka hapa tulipofikia. Basi tulipokuwa chumbani nikawa sina amani, nikamwambia mume wangu kwani kuna nini, akaniambia tusalikwanza maana hatujasali. Ilikuwa juzi Ijumaa nilikuwa fellowship mchungaji akanipigia simu akaniambia njoo officen kwangu, alipoenda akamkuta Yule mchungaji ambaye lile eneo tulilinunua kwake, tukawa tumeelewana tulipe milioni 25 ili kufidia kile kiwanja ndugu yake kutoka Arusha amekuja yupo pale kwa mchungaji. Yule baba akasema kwa kweli hii imeshakuwa ni laana katika ukoo wetu, hatutapenda kitu kama hiki kitokee wala hatutaweza kujenga wala kuishi kwenye nyumba hii, akasema kesho Jumatatu tutakuja hapa officen Mr. Kimaro utakuja na mke wako na nyie wengine mtakuja tukutane hapa, tunataka hili tatizo liishe kuna kiwanja kipo Tabata Segerea tutaenda kukiangalia, tutapatana na Yule mtu mtanunua mumfidie Yule mchungaji kile kiwanja, ambacho Yule mchungaji tulikabidhi milioni 15 na risiti tunazo. Kwa hiyo Mungu wa Nabii Flora ameenda kutenda miaka 4 ambayo tuliishi kwa mateso.

JASMINI ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA VIRUS VYA UKIMWI BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Jasmini John naishi Manzese; kwa kweli madhabahu hii ni ya hatari na inatisha, napenda kuwaambia muamini na kukubali Mwenyezi Mungu atawajalia, watoto wangu wadogo nimewazaa katika mazingira ya HIV. Lakini juzi kwa uwezo wa madhabahu hii, nampenda Nabii Flora kwaajili ya sabuni hii, Jumapili hadi Jumatano kwenda kupima nikakuta Negative. Nilikuwa na Virusi vya UKIMWI na watoto wangu toka mwaka 2009 mpaka 2014, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa kuniponya

JULIUS ANAMSHUKURU MUNGU KUMWEZESHA KUAPA FEDHA ALIZOKUWA ANAZIITAJI


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Julius; tarehe 27 mwezi uliopita kuna kazi ilikuwa ifanyike inaitaji shilingi milioni nane, lakini nikakosa kabisa zile pesa, nikampigia mama mchungaji Ansila nikamwambia nahitaji shilingi milioni 6, akapeleka simu kwa Nabii, nikamwambia Nabii mimi nataka pesa shilingi milioni 6, Nabii akaniambia nakuombea upate hizo pesa. Siku ya Alhamisi nikakuta mtu ameniletea milioni 4, Ijumaa mwingine akaleta milioni 4 kwa hiyo zikawa milioni 8, kwa kweli nilishukuru sana nimepata milioni 8 badala ya milioni 6, kwa kweli mama amenisaidia sana.

MAMA MCHAKI ANAMSHUKURU MUNGU MWANANE BAADA YA KUTUMIA STICKER AMEWEZA KUPATA KAZI YENYE MSHAHARA MZURI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mama Mchaki; namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa mambo aliyonitendea kuhusu sticker na sabuni, kulikuwa na mtoto wangu alipata kazi bila kufanya interview. Hii sticker ni ushuhuda mkubwa sana kwangu, nilimnunulia nikasema kwa sababu wewe hupati nafasi ya kuja Kanisani kwa Nabii Flora, naomba niwe napeleka maombi yangu mbele, nasali hapa kwaajili ya mtoto wangu. Lakini mwenyezi Mungu alivyonitendea siku ya Jumatano jioni, muda wa saa kumi na mbili alipata simu kwamba anaitajika kwenda kufanya interview. Alipokwenda kwenye interview nikamwambia hii sticker utakwenda nayo, utakapokuwa unafanya interview utajiambatanisha na Nabii Flora, kweli akasema mimi nilipokuwa nafanya interview nilijiambatanisha na Nabii Flora, na sabuni niliogea, na maji niliogea na kuyanywa, nikamwambia usichoke. Alienda siku ya Alhamisi kufanya interview, kufika saa tatu wakampigia simu kwamba umepata kazi, na ambayo namshukuru mwenyezi Mungu, kule alipokuwa mara ya kwanza walikuwa wanamlipa mshahara mdogo sana, lakini sasa hivi alipokwenda wamemzidishiwa mara tatu. Kupitia sticker hii, napenda kuwaambia Watanzania wote mje hapa kwa Nabii Flora, Mungu wa Nabii Flora anatenda kila kitu unachokiomba.

NEEMA LUKAS ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA UVIMBE KWENYE KIZAZI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Neema Lukas ; Bwana amenitendea miujiza mikubwa, nilikuwa na uvimbe katika mfuko wa uzazi, nilipokwenda Hospitali nikaambiwa nina uvimbe centimeter 2.5, mara ya pili nilivyoenda nikaambiwa ninauvimbe centimeter 3.47, kwa maana hiyo inabidi nikafanyiwe operation. Kuna mtu akaniambia usiende Muhimbili nenda Salasala kuna dada mmoja anaitwa Nabii Flora watu wanapo. Nikaja hapa, Nabii Flora siku hiyo ya kwanza akaniombea, siku hiyo hiyo ya kwanza akaniambia uvimbe umekwisha, niliondoka nikarudi nyumbani. Tarehe 10 nikaenda tena Hospitali, Daktari aliponipima akaniambia mbona hauna uvimbe, namshukuru sana Mungu, napenda kuwaambia watu wengine Nabii Flora anatenda.

PILI MOHAMED ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA MWANAE BAADA YA KUTUMIA MAJI YALIYOOMBEWA NA NABII FLORA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Pili Mohamed; mimi nilikuwa mtu wa shetani, lakini baada ya kufika hapa kwa Nabii Flora, nimepata kuinuka na kulijua neno la Mungu. Pia nyumbani kwangu wanangu walikuwa hawaishi kuumwa, kama Jumapili iliyopita mwanangu alikuwa anaumwa sana, mume wangu akaniambia tumpeleke kwa mganga, mimi nikamwambia siwezi kwenda nina Mungu wa Nabii Flora nitamtumia.

Nikachukuwa maji nikamuogesha mwanangu na kumnywesha, sahiyo hiyo akatapika akapata fahamu, nikamwambia mwanangu kinachokuuma ni nini, akaniambia nilipita njia panda nikaokota mia hamsini, nilivyoitumia nilijisikia kizunguzungu nikadondoka. Akaniambia mahali hapa nilipofikia namshukuru Mungu wa Nabii Flora na Kanisani twende wote, na mwanangu nipo naye hapa hapa Kanisani, nashukuru sana haya maji yamenitendea sana.

DADA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MDHAMINI KWAAJILI YA KAZI YAKE YA MUZIKI WA INJILI

Bwana Yesu asifiwe; namshukuru Mwenyezi Mungu wa mahali hapa anatenda makubwa, Jumapili iliyopita nilikutana na mtumishi wa Mungu Nabii Flora, nikamweleza kuhusu matatizo yangu, nikamwambia nimechoka kuitukuza dunia. Sasa kwa nini hii sauti nzuri iendelee kutukuza walimwengu wakati yeye aliyenipatia hii sauti nishindwe kumuinua, nahitaji sasa hivi kumtukuza ila sina uwezi, nimetengeneza sasa hivi nyimbo moja. Nabii akaniambia hii wiki haitapita utapata mfadhili, alipokuja huyo mfadhili siku ya kwanza alikuwa ananishangilia tu hakuniambia chochote, siku ya pili akaniambia dada unasauti nzuri kuanzia leo mimi nitakuwa mfadhilia wako. Nikasema Mungu wangu ambaye anamuinua Nabii Flora mahali alipo pale Salasala wakati huu akipiga goti lake yeye kwaajili yangu mimi basi akubariki wewe kazi yako ya mikono unayofanya, huku unakokwenda urudi basi akubariki na wewe uweze kunibariki. Akaniambia naenda Iringa kununua uwanja mkubwa sana kwa sababu ya kazi zangu, nikirudi uniambie mahitaji ya studio ni shilingi ngapi ili niweze kukudhamini

MAMA ANAMSHUKRU MUNGU WA NABII FLORA MWANAE ALIKUWA ANAUMWA BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA AKAPONA


Bwana Yesu asifiwe; nashukuru Mungu katika madhabahu hii ya Nabii Flora, juzi nilipigiwa simu mwanangu yupo Hospitalini maututi, nilikuja hapa nikamuona Nabii nikamwambia mwanangu anaumwa sana, pressure imeshuka na pia anaumwa na kichwa hajui afanye nini. Baada ya Nabii kuomba alipata nafuu na alitolewa Hospitali siku hiyo hiyo, namshukuru sana Nabii Flora chakumpa sinaa, ananisaidia sana katika familia yangu.

JINSI YA KUFIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASLA KWA NABII FLORA PETER

Kama unatokea Mwenge, panda magari ya Tegeta, shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisani kwa Nabii Flora peter

Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com

No comments:

Post a Comment