“HAPA nilipo mimii ni kwa neema ya Mungu, vile nilivyo mimi ni kwa neema ya Mungu, nimetoka mbali-toka mbali toka mbalii nimetoka mbaliii…… Ni kwa neema tu na rehemaa, ni kwa neema tu na rehemaa.”
Hayo ni baadhi ya maneno katika
wimbo wa ‘Ni kwa Neema na Rehema’ uliomtambulisha vema kijana Edson Mwasabwite, ambaye kwa sasa ana albamu moja yenye jumla ya nyimbo nane ikibebwa na wimbo huo, huku akiwa mbioni kukamilisha albamu yake ya pili.
wimbo wa ‘Ni kwa Neema na Rehema’ uliomtambulisha vema kijana Edson Mwasabwite, ambaye kwa sasa ana albamu moja yenye jumla ya nyimbo nane ikibebwa na wimbo huo, huku akiwa mbioni kukamilisha albamu yake ya pili.
Albamu hiyo yenye nyimbo za kutia faraja, kusifu na kuabudu ilianza
kupendwa mkoani Iringa na Mbeya ambako watu wengi hupenda kusikiliza
wimbo wa ‘Ni kwa Neema na Rehema’.
Akiwa ametambulishwa vema na albamu hiyo, Mwasabwite anasema ana kila
sababu ya kumshukuru Mungu alipofikia kwa kuwa amekutana na changamoto
nyingi sana wakati anaanza kuimba
kama mwimbaji binafsi.
kama mwimbaji binafsi.
Edson aliachwa yatima kwa kuondokewa na wazazi wake ambapo wimbo wa
‘Ni kwa Neema na Rehema,’ amesema amejaribu kuelezea jinsi neema na
rehema ya Mungu ilivyomtetea na kumfikisha alipo, maana asingekuwa
Mungu labda ingebaki historia tu kutokana na maisha magumu aliyopitia.
Amesema yeye ni kijana aliyeokoka, anampenda Mungu, anaabudu katika
Kanisa la Kilutheri Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Kilio chake Edson kwa waimbaji wenzake ni kuwasihi kuwa barua inayosomwa vema na wanaowahubiria
ili maneno na matendo yawe sawa na kubariki pamoja na kuwavuta watu
kwa Yesu zaidi kuimba kwao isiwe hapa duniani pekee bali siku moja wakajiunge na jeshi kubwa la malaika mbinguni.
ili maneno na matendo yawe sawa na kubariki pamoja na kuwavuta watu
kwa Yesu zaidi kuimba kwao isiwe hapa duniani pekee bali siku moja wakajiunge na jeshi kubwa la malaika mbinguni.
Edson anawasihi waimbaji wasiwe kama vibao kuishia kuonesha njia wakati vyenyewe haviendi huko kunakotakiwa.
Anasema kuwa hafungwi kuabudu katika kanisa lolote na ikiwa atapokea maono ya kuhama, basi atafanya hivyo.
Anasema wimbo wake wa ‘Ni kwa Neema na Rehema’, aliimba kwa sababu
hakutarajia kama angefika alipo, kwani ni kwa neema tu, kwakuwa aliishi
maisha magumu baada ya kuachwa yatima.
“Hii ni historia ya maisha yangu. Wokovu wenyewe ni kwa neema, nikiangalia vijana wengine mimi niko salama zaidi,” anasema.
Mafanikio
“Mafanikio yapo, japo kwa mtu mwingine yanaweza kuonekana kama
sifuri, ila mafanikio inategemea na huyo mtu yuko katika nafasi au
ngazi gani. Ingawa ndiyo nimeanza, naona mafanikio, namshukuru Mungu,”
anasema.
Changamoto
Edson anasema changamoto katika uimbaji zipo, hasa kwa chipukizi,
kwani mtu anapoanza kuimba unakuta hana fedha, mara nyingine inakuwa
ni kikwazo ili kuweza kuweka uimbaji katika viwango vya juu.
Anasema changamoto nyingine ni watu wengine kushauri vibaya kwa makusudi ili uanguke.
“Hakuna ushirikiano kwa wale walio wazoefu katika muziki wa Injili,
hii imesababisha hata hasara, kwa kuwa unakosa mwongozo kutoka kwa
wazoefu.
“Lakini pia kuna changamoto ya utaalamu, wasikilizaji na jamii kwa
ujumla hawajaupa nafasi sana muziki wa injili. Watu wengi wanauchukulia
kama burudani tu, suala la kuelimisha na kusisimua.
“Ila tunashuru Mungu kwamba watu wanatuunga mkono. Ndiyo maana
utakuta nyimbo zinazohit ni zile za kuburudisha zaidi. Kwa Tanzania
Mungu ameupa muziki wa Injili Neema,” anasema.
Anaongeza kuwa, kwa sasa anaishi Dar es Salaam. Kuhusu suala la kuoa
anamuomba Mungu ampe mke mwema, kwani ni heri ukosee kujenga nyumba au
kurekodi wimbo utaurudia lakini si kuoa.
Ushauri
“Ujumbe wangu kwa waimbaji wenzangu wa nyimbo za
Injili, wajue kama unahubiri, uwe mfano na wakili, tusiwe kama vibao,
lakini tusiende huko. Yesu alisema itamfaa nini mtu apate vya dunia na
kuikosa mbingu.
“Wito wangu kwa watu wote ni wawe tayari kuelimishwa pia na nyimbo
za Injili na si kuburudika tu, wajue tunaishi kwa neema tu, wajue Mungu
ndiye ametupa vyote tulivyo navyo, ambao hawajaokoka wampokee Yesu
Kristo.
Vyote tulivyo navyo bila Kristo ni bure, wajiulize wataishi wapi baada ya maisha haya.
“Tuwe barua, mtu akituona ajue kweli huyu anamwimbia Mungu aliye hai.
Tujiandae kuimba mbinguni, si kupata sifa hapa duniani na kwa waimbaji
chipukizi, kwa wanaoanza wasikate tamaa, kwani hakuna aliyezaliwa
akiwa na jina, wala vitu, wawe wavumilivu na waaminifu mbele ya Mungu
ili wafanikiwe,” anasema.
Historia
Edson alizaliwa Meta, Mkoa wa Mbeya, Aprili 24, 1983 na kupata elimu ya msingi Mtaba.
Anasema kuwa kipaji chake cha uimbaji kilitambuliwa akiwa Shule ya Jumapili ‘Sunday School’ Rungwe, mkoani Mbeya.
Anasema kuwa katika familia yao wamezaliwa watoto watatu kwa upande wa mama yake.
Anaeleza kuwa yeye ni mtoto wa nje ya ndoa na alilelewa na mama yake,
ambapo hakumfahamu baba yake hadi alipofika darasa la nne.
“Nimeishi maisha magumu sana yenye changamoto za kila aina, yaani
unaishi na mama ambaye ni mkulima, maskini na kama unavyojua maisha ya
kijijini wakati mwingine hakuna kula, kuni zimelowa au kukosa hela ya
chakula,” anasema.
Anasema kuwa baada ya kumfahamu baba yake alikaa naye kwa miaka
mitatu na akafariki dunia mwaka 1999 na ndipo matumaini ya kusoma
yakapotea. Anaeleza kuwa miaka michache baadaye mama yake alianza
kuugua.
“Nilimuuguza mama yangu huku nikilea familia, aliugua kwa muda wa
mwaka mmoja na nusu na alifariki dunia mwaka 2005, yaani hapo ndoto
zote zilikufa, ila namshukuru Mungu maana mimi niliokoka mapema,
ilinisaidia kutokujiunga katika makundi ya kihalifu, maana hofu ya
Mungu ilikuwa ndani yangu,” anasema.
Mbio za umaarufu
Anasema kuwa mbio zake za uimbaji zilianza rasmi mwaka 2007 na kuanza kutafuta michango, lakini hakupata.
“Kuna watu siwezi kuwasahau, walinisaidia sana katika harakati zangu
za uimbaji, yaani mtu kama Angonile, Sifa Mwankili na Mama Nisa, hawa
walikuwa wakinipatia fedha na hata kunikopesha, ila sikufanikiwa na
nikarudi kijijini,” anasema.
Anaeleza kuwa baada ya mwaka huo kutofanikiwa alirejea tena Dar es
Salaam 2010 akiwa hana mfadhili, anasema kuwa maisha yalikuwa magumu
sana japo alifanikiwa kurekodi albamu hiyo.
“Baada ya kurekodi, nilirudi nayo kijijini na ndipo niliugua TB,
nikatibiwa na kupona, lakini maisha yakawa ya taabu sana, nikawa sina
hela, madeni mengi, kazi haipo sokoni, ninayo ndani,” anasema.
Anasema hawezi kumsahau Ephraim Mwansasu, kwani ndiye aliyemsaidia
kumpeleka kwa wasambazaji na albamu hiyo ambayo inapendwa na wengi.
Usiyoyajua
-Muimbaji huyo hajaoa, hana mtoto.
-Albamu yake ya ‘Ni Kwa Neema na Rehema’ aliirekodi mwaka 2010.
-Alikuwa akifanya biashara ya kahawa mbichi.
-Kanisa halikumkubali na kipaji chake
-Maisha yake yote hakujua wala kuhisi kama angekuwa maarufu.
-Ni yatima.
-Wamezaliwa watatu, wa kiume wawili na wa kike mmoja.
-Alisaidiwa na rafiki zake kuweza kuingia studio.
-Aliokoka mwaka 2001.
-Aliishi akilea familia ya watu saba.
-Wasambazaji ndio wapanga bei ya kazi.
Albamu
Albamu yake ya kwanza ina nyimbo nane ambazo ni ‘Ni Kwa Neema na
Rehema’, ‘Tarajia Mujiza’, ‘Asante Yesu’, ‘Usiwe Mbali Nami’, ‘Bwana
Yesu’, ‘Atanifuta Machozi’, ‘Milele Usifiwe’ na ‘Mungu Wetu Anaweza’.
Akizungumzia ujio wa albamu yake mpya, Edson anasema itakuwa na wimbo ambao utatoka Desemba
mwaka huu.
mwaka huu.
Anasema albamu hiyo itaitwa kwa jina la ‘Amenihurumia asilimia mia’,
ikiwa pia na nyimbo kama ‘Nikiwa na umri wa miezi Nane’, ‘Kweli ni
Mimi’, ‘Mkono Wako’, ‘Uwe Nami’, ‘Nitamwimbia Bwana’, ‘Wewe ni
Mshindi’, ‘Mtetezi Wetu yu Hai’, ‘Tumia Vizuri Nafasi’ na ‘Kyala
Nnunu’.
Anasema kuwa albamu hiyo ameirekodi Cke Studio ikiwa na mahadhi
mbalimbali kama rhumba, kwaito, zouk na sebene na itasambazwa na Umoja
Vision.
Kuhusu wapenzi na mashabiki wa Morogoro kumhitaji katika Tamasha la
Krismasi, litakalofanyika Uwanja wa Jamhuri, Desemba 26, anasema bado
hajapata mwaliko wa kushiriki.
Lakini anasema kwa vile ni tamasha kubwa la kumwimbia Mungu,
angefurahi kama angepata nafasi hiyo ya kujumuika na wengine siku hiyo.
“Nawashukuru wapendwa, wapenzi na mashabiki wa nyimbo za Injili wa Morogoro kwa kunikubali, lakini
sijapata mwaliko,” anasema Edson.
sijapata mwaliko,” anasema Edson.
Hata hivyo, anadokeza kuwa aliwahi kupigiwa siku na waratibu wa
tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotions, lakini bado anasubiri
mwendelezo.
Tamasha hilo litakaloanzia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Desemba 25, mbali ya Morogoro litafanyika pia Kilimanjaro, Dodoma na
Arusha.
No comments:
Post a Comment