DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Wednesday, January 22, 2014

MESS JACOB CHENGULA ALIVYOSHUSHA WINGU LA UTUKUFU KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B

Asemavyo bloga, Rulea Sanga
Hakika ukiangalia hii clip utaamini kuwa watu wamezipokea nyimbo za Mess Jacob Chengula kwa mikono miwili. Watu wamejiachia katika clip hii, wakicheza bila steps ili mradi sifa na utukufu zimrudie Mwenyezi Mungu. Ukiangalia kwa makini utaona hata Mess Chengula mwenyewe alifika point akawa haamini watu walivyoupokea wimbo wake "MUNGU WETU HABADILIKI|"
Mess Jacob Chengula

Sipati picha hiyo siku ya tarehe 2 Machi 2014 katika ukumbi tulivu wa UBUNGO PLAZA hapa jijini Dar es Salaam, hapatakalika kabisa siku hiyo!!. Ninakusihi  usikubali wala kuwaza kupanga kutofika ukumbini kwa maana utakosa mengi kutoka kwa Mtumishi wa Mungu aliyekubalika machoni pa watu na mbele za Mungu kwa huduma yake hii ya uimbaji. Ukiangalia kwa makini katika clip hii utaona Mess Chengula alivyodata badala ya kupokea pesa wanazomtunza akaanza kurusha pesa kwa wadau. Hii ina maanisha mtumishi wa Mungu anafurahia sana kufanya kazi ya Mungu kuliko kupenda pesa.

Kitu kingine ambacho kinanichanganya katika albamu hii ni vile Mess Jacob Chengula alivyo-shoot albamu yake katika nchi mbalimbali kama Hong Kong, China, Dubai na Tanzania. Kama mdau wa nyimbo za injili na mzalendo wa nyimbo zetu za kibongo,  unafikiri humo ndani mna utamu wa aina gani?  Ninakusihi mtu wa Mungu usikose kujipatia albamu hii siku ya tamasha la uzinduzi ili ujionee watu wanapokuwa kuwa serious kwa kazi ya Mungu.

Mess Jacob Chengula na dancers wake
Mbali na hayo yote, lingine ni juu ya waalikwa watakaosindikiza tamasha hili la fungua mwaka 2014. Mess Jacob Chengula ameweza kualika waimbaji zaidi ya 20 watakaoimba siku hiyo. Ki ukweli binafsi nimeona matamasha lakini hili kiboko kwa kuwa na waimbaji wengi namna hii na ni waimbaji wale ambao wana majina makubwa Afrika Mashariki na dunia. Kutakuwa na Rose Muhando, Bony Mwaitege, Masanja Mkandamizaji, Neema Gasper, Ibrahimu Sanga, Silas Mbise wa Wapo Radio, AtoshaKissava na wengine wengi.
Mess Jacob Chengula hakuishia hapo pia ameaalika mabloga kama akina sisi, Rumafrica na wengine wengi watakaofika siku hiyo.

Kutakuwa na kiingilio katika tamasha hili. VIP ni Tshs 10,000 na viti vya kawaida ni Tshs. 5,000. Tamasha la uzinduzi litaanza saa sita mchana ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mh. Januari Makamba.


DVD ya Mungu Habadiliki ya Mess Jacob Chengula.




Creativity Rumafrica +255 7158523
www.rumaafrica.blogspot.com






No comments:

Post a Comment