DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Thursday, February 13, 2014

NABII FLORA PETER AHUBIRI SIKU YA JUNAMNE 11.02.2014 KUTOKA KATIKA KITABU CHA YEREMIA - SOMA UJUMBE HUU UTAKUBADILISHA

Karibu sana mwana wa Mungu, karibu sana Mtanzania katika huduma ya maombezi, tunamtukuza Mungu katika huduma hii, hatubagui dini wa dhehebu tunamkaribisha mtu wa kila aina. Mimi na mtumishi wangu tunakusalimu kwa jina la Bwana, mtazamaji wetu unayetutazama kwenye youtube na kutusoma kwenye blogu na facebook, tunasema Mungu ni mwema kila wakati.
UJUMBE WA NENO LA MUNGU UNATOKA KATIKA KITABU CHA YEREMIA 31:10
Kabla Nabii ajaanza kutupa ujumbe wa leo, anatueleza kwanza habari za mwaka huu, katika kitabu cha Mwanzo 26:12
Isaka alipanda mbegu alipoingia katika nchi ile, akavuna mara mia moja kwa kipimo kimoja, akawa mkuu tena mkuu sana.
Yeremia 31:10
Biblia inasema
: Sikilizeni neno la Mungu enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali mkaseme, aliyemtawanya Israeli atawakusanya; yaani aliyekuwa anakutawanya, anatawanya mafanikio yako, watoto wako wamepota katika mazingira ya kutatanisha, ametawanya bahati zako, lakini leo yule Bwana wa Israeli anakwenda kukusanya baraka zako. Huu ni mwaka wa urejesho, kama ulipoteza baraka zako zinakwenda kukusanywa, tunakusanya mafanikio yako tunakwenda kurejesha, miaka yako iliyoliwa na madumadu,na parare tunakwenda kuirudisha.
Biblia inasema: Nakulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake; anasema Bwana anakwenda kukulinda wewe kama mchungaji anavyolinda kundi lake, anakusanya baraka zako zilizokuwa zimetekwa, Bwana wa Israeli anasema anakenda kukusanya vitu vyako vilivyopotea. Yamkini umepoteza simu, laini, mafanikio, bahati zako, umepoteza mwanao katika mazingira ya kutatanisha amekufa bila sababu, majirani wanamuona, wewe mwenyewe anakubishia hodi, anakwenda kukusanya Bwana, huu ni mwaka wa marejesho na wiki ya marejesho anakwenda kurudisha.
Biblia inasema: Atakwenda kukusanya na kulinda, kwa maana Bwana amemuweka huru Yakobo; anasema atakwenda kukusanya vitu vyotevilivyopotea, anasema kwa maana Bwana amemuweka huru Yokobo, Yakobo ni mtumishi wa Mungu, na mimi nimewekwa huru na Bwana, Kanisa limewekwa huru, alisema Bwana nitamuweka huru Yakobo.
Biblia inasema: Amekukomboa katika mkono uliohodari tena hodari kuliko yeye; yaani Bwana ametukomboa sisi kwa mkono uliohodari, tena mkono ulio hodari kuliko yeye, hata kama wachawi walitufunga upo mkono hodari kuliko wachawi. Upo mkono hodari kuliko Kansa, UKIMWI unakwenda kukutoa, unakwenda kufunguliwa, hakuna jambo lisilowezekana, hujapokatwa na kuanguka mchangani, kwa harufu ya neno utachipuliwa tena. Anasema nitaitikisa mbingu, bahari na nchi kavu, na vyote vitamanishavyo nitaviamuru vije kwako, kama ni mali, dola vitakuja Bwana ataleta baraka.
Biblia inasema: Nao watakuja wakiimba kama mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa Bwana; anasema nao watakuja wakiimba kama mlima Sayuni, walikudharau, kubeza na kusema tuone kama atafanikiwa watakuja kwako kuimba, maana Bwana anakwenda kufanya vitu vya tofauti katika maisha yako, maana huu ni mwaka wa urejesho, na hii ni wiki ya kurejeshewa.
Biblia inasema: Wataukimbilia wema wa Bwana, na fedha, nafaka na mafuta, na wachanga wa kondoo na wachanga wa ng’ombe, Roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji, wala hawata huzunika tena kabisa; huu ni mwaka wa kujibiwa, usikae nyumbani shtuka, ni mwaka wa kurejeshewa baraka zako, na Bwana anasema mwaka huu sio kama ile miaka tuliyoipitia, ambao tulikuwa tunamwagilia kwa mipira, huu ni mwaka ambao unatunzwa na Bwana. Huu mwaka 2014 unaongozwa na Yesu Kristo mwenyewe, anasema atakuwa nasi mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka, hakuna kifo, misiba, huzuni imefungwa kuzimu.
Biblia inasema: Nikasikia maneno yako wakisema, hakika huu ni Mwerezi wa Lebanoni, uliopandwa kando ya mto tena unastawi majira yote. Bwana atakupa nafaka, divai na mafuta; watakuita wewe ni Mwerezi wa Lebanoni, maana umepandwa kando kando ya vijito vya maji, wakija tarehe moja, kumi watakutana na majibu, wakija wachawi watakukuta umejaa upako, wakikugusa wanapigwa shoti.

JINSI YA KUFIKA KANISANI
Kama unatokea Mwenge, shuka katika kituo cha Mbezi Mbuyuni na uliza kanisani kwa Nabii Flora

Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com

No comments:

Post a Comment