Alikuwa na haya ya kusema:-
Sasa nimeamini ya kwamba ukiwa mpambanaji na unafanya mambo yako kwa
bidii, Mungu atakusogeza hatua nyingine. David Robert ni classmate wangu
(Rulea Sanga) tumepiga kitabu wote Jitegemee tukichukua course moja ya
HGE miaka ya 2002. Davi alikuwa kichwa balaa na alikuwa anapenda sana
kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Davi alipenda sana kupiga kikapu
yaaani mchezo wa basketball tukiwa Jitegemee High School, kipindi hicho
Mh. Masawe alikuwa Headmaster wetu.
Muimbaji wa Muziki wa injili David Robert akiwa na Balozi Mulamula.Ziko picha zingine hapa
Muimbaji wa Muziki wa injili David Robert akiwa na Balozi Mulamula.Ziko picha zingine hapa
Hakika ukimtumikia Mungu kwa Roho wa kweli, na kwa akili zako na mali zako ipo siku na YEYE atakushangaza. Leo hii David Robert anakaa na wakuu na kufanya nao mipango ya dunia, jamani hili sio jambo dogo kwa akili ya kibinadamu.
Tuzidi kumuombea sana ndugu yetu atakapokuwa anachangia maada mbalimbali zikakubaliwe na kuonekana zinachachu katika dunia hii. Tumuombee awe na busara na hekima anapoongea na wakubwa katika mikutano yao. Mungu na akubariki sana wewe utakayemuombea ndugu yetu.
David Robert na mke wake
No comments:
Post a Comment