DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Thursday, February 6, 2014

SHUHUDA ZA KUINUA IMANI YAKO KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA

EMMA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI



Bwana Yesu asifiwe, naitwa Emma Immanuel; madhabahu hii ya mtumishi Nabii Flora imenitendea makuu, nilikuja hapa toka mwaka juzi mwezi wa kumi na moja. Nilikuwa nina Saratani ya shingo ya kizazi, nikamueleza mtumishi akaniambia nije kwenye maombi, nikawa kila nikija maji yanatoka, akaniambia nije siku 21. Nikaja hapa siku 21, nilipoenda Moshi kupima wakaniambia hawalioni tena hilo tatizo, kwa hiyo Madaktari wameniambia nirudi mwezi wa nne. Nilipoenda walikuwa wanichune kizazi, basi wakakuta tatizo hakuna, nilimshukuru Mungu kwa kushuka pale kitandani sijafanyiwa operation, napenda kuwaambia Watanzania wenzangu msikate tamaa, mahali hapa panauponyaji, mkiwa na shida yoyote mwambieni Mungu wa Nabii Flora.

GLORY ANAMSHUKUU MUNGU WA NABII FLORA BAADA YA KUNUNUA STICKER YA NABII FLORA NA KUIWEKA NYUMBANI KWAKE, KULIKUWA KUNA MBU SANA LAKINI SASA WAMEKWISHA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Glory; namshukuru Mungu wa madhabahu hii, kupitia mtumishi wa Mungu Nabii Flora, nilinunua sticker ya Nabii Flora.

Namshukuru Mungu kwa jinsi ya ajabu, nyumbani kwangu kulikuwa kuna mbu sana, hata kama ukipulizia dawa lazima ufunge neti ndio ulale, lakini sasa hivi hatufungi neti na mbu hakuna. Kweli Mungu ni wa ajabu, Mungu anaonekana kupitia sticker za Nabii Flora, unatakiwa kuwa na imani tu.

HADIJA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA VIRUSI VYA UKIMWI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Hadija Abdala; namshukuru Mungu wa madhabahu hii ameniponya UKIMWI, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora, nilijisikia furaha sana baada ya kwenda kupima nikakuta nimepona. Napenda kuwaambia Watanzania wenzangu wasikate tamaa Mungu wa Nabii Flora anaponya, Mungu abagui dini wala kabila kwa hiyo wote wenye matatizo mbalimbali waje watapona.

JOYCE ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA MAMA YAKE ALIPOTEA AKIWA CHIZI, LAKINI BAADA YA KUMLETA KWA NABII SASA AMEPONA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Joyce; Mungu amenitendea, mama yangu alipotea mwezi wa kumi na mbili huko Bukoba, nilikuja naye hapa akiwa chizi. Lakini sasa hivi namshukuru Mungu, anaweza kuogesha watoto, anapika, anafua, namshukuru sana Mungu wa madhabahu hii.

JULIUS ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMUWEZESHA KUPATA GARI MPYA

Bwana Yesu asifiwe, naiwa Julius; mimi nilikuja hapa nikiwa nimeuza vitu vyangu vyote, Nabii Flora alianza kuniombea nikiwa na simu moja. Lakini Mungu amenitendea makuu sana, japokuwa nilikuwa sina kitu lakini niliweza kupata magari 5. Pia namshukuru Mungu nimepata gari linguine zuri sana na la gharama sana



KAKA ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KULIPA DARASA LAO USHINDI KATIKA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

Bwana Yesu asifiwe; namshukuru Mungu wa Nabii Flora kwa kuliwezesha darasa langu kwa kuchukuwa ubingwa wa chuo, mimi ni mbunge wao katika chuo cha Ustawi wa Jamii, namshukuru sana Mungu kwa kutupa ushindi.

MAHIMUNA HAMISI ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA MATATIZO YALIYOKUWA YANAMSUMBUA KWA MUDA MREFU, NA PIA BABA YAKE AMEOKOKA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mahimuna Hamisi; napenda kumshukuru Mungu wa Nabii Flora kwa matendo makuu aliyonitendea, katika maisha yangu nilianza kuumwa nikiwa na miakab 3, lakini sikutegemea kama ningepona, na mimi ningeweza kutembea naachiwa peke yangu. Nilikuwa siruhusiwi kutembea peke yangu, kwa waganga kote tumemaliza lakini siponi, baada ya kuangaika sana ndio nikaelekezwa mahali hapa. Nilifika hapa siku ya Alhamisi, namshukuru Mungu baada ya kuombewa nimepoa, na pia namshukuru Mungu kwa kunipa mama, Nabii Flora, Mchungaji, July na Ansila, kwa maana nilipofiwa na mama yangu nilihuzunika sana. Namshukuru Mungu pia baba yangu ameokoka yupo Arusha, siku moja nilipelekwa kwa Mchungaji July, baba yangu akasema sitaki ulale huko, basi mchungaji July akanichukuwa nikawa nakaa kwake. Tukawa tunashindana, sasa juzi akawa ameenda kwa waganga wa kienyeji, kulikuwa na msiba wa dada yangu amekufa, kwa yule mganga wakamwambia hatukutaki tena. Akaondoka akaenda Roma, kule akawa anasema anaungua tu, akawa anakimbia, yaani kila sehemu anayokaa anakimbia kimbia tu, kwa hiyo sasa hivi ameokoka akakataa jina la mzee Hamisi kwa hiyo sasa anaitwa Moleli Tobias.

MICHAEL ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUPATA KIBALI CHA KURUDI NCHINI KWAKE

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Michael; kupitia madhabahu hii ya Nabii Flora Mungu amenitendea miujiza, nilikuwa nasubiria barua ya kurudi nje ya kanda mahali ambapo nilikuwa ninaishi, kwa kweli niliona giza njia ilikuwa imefungika. Lakini toka nimekuja kuabudu mahali hapa, nina wiki mbili sasa, na nilipokuja niliongea na Nabii Flora nikamuelezea shida zangu, lakini alinielezea mambo ambayo yalinishtua. Siku ya Jumatano nilikuja hapa morning Glory, baada ya hapo nilienda wizara ya mambo ya ndani, kwa sababu nilisubiria barua kwa muda mrefu. Nilienda nikiwa nimebandika sticker yangu kwenye bahasha niliyokuwa nimebebea document , nilipoingia nikaongea na director akaniandikia barua ya kuwakilisha chama cha umataifa, siku 30 waniondoe Tanzania. Sasa nasubiria, siku ya Jumatatu au Jumanne chama cha mataifa waniambie ni siku gani nitarudi nchi ya Kanada. Naapenda kuwaambia kwamba msiwe kama Tomaso aliyesema hawezi kuamini kama hajaona.

RICHARD ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA MAMA YAKE ALIKUWA ANAUMWA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Richard Masumbwi; Mungu wa Nabii Flora amenitendea makuu, mama yangu alikuwa anaumwa, nikaja kwa Nabii Flora akamuombea mama yangu akapona, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora.

ROSE ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMUOKOA KATIKA AJALI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Rose, mimi ni mwenyeji wa Kunduchi; Mungu ameniokoa katika ajali, ilikuwa ni siku ya Ijumaa juzi. Kuna sehemu nilikuwa naelekea, ghafla gari ikadumbukia kwenye mtaro, tulishindwa jinsi ya kutoka, lakini namshukuru Mungu wote tumetoka wazima hakuna aliyeumia hata mmoja.

ROSE ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLOA BIASHARA ZAKE ZILIKUWA HAZIENDI LAKINI BADA YA KUJA KWENYE MAOMBI SASA BIASHARA ZIPO VIZURI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Rose; nilikuja hapa nikiwa nalia hata Nabii alinionea huruma, namshukuru Mungu wa Nabii Flora amenitendesa, biashara zangu zilikuwa zimefungika, yaani nilikuwa sipati faida yoyote, hata pesa ya kula nilikua nakosa, lakini sasa hivi namshukuru Mungu sasa hivi zimefunguka. Napenda kuwaambia Watanzania wenzangu kwa Mungu hakuna kitu kinachoharibika, ukimuona Nabii Flora kila kitu chako kitafunguliwa

SALUM JOCOB ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMUWEZESHA KUFAHULU MTIHANI WA KIDATO CHA PILI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Salmu Jacob; namshukuru Mungu nimefahulu mtihani wa kidato cha pili, nilikuja hapa mwaka jana kwenye maombi. Nilikuja hapa mwaka jana Nabii akaniombea, akasema nitafahulu, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora.

THOMAS MICHAEL ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMWEZESHA KUPATA KODI YA KULIPIA CHUMBA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Thomas Michael; mimi nilikuwa nimeshashindwa nawaza kurudi Kijijini kwa sababu hata kodi ya kulipia chumba nilikuwa sina. Baada ya kufika hapa Nabii aliniombea, na hapo hapo nilipigiwa simu nikapewa pesa ya kodi, Nabii pia aliniambia Mungu ataniinua juu, namshukuru Mungu sasa hivi nina mialiko mpaka nashindwa nijigawe vipi.

ZUHURA HAMIS ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMLINDA NA MAADUI ZAKE

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Zuhura Hamis; namshukuru Mungu wa madhabahu hii, amenitendea mambo ambayo sikutegemea kabisa, nilikuwa naishi sehemu moja inaitwa Kongowe, majirani zangu wamenisumbua kwa muda mrefu sana wakiniloga mimi na mtoto wangu. Nikaja hapa kwa Nabii Flora nikamueleza, Nabii akaniambia nisihame pale nikae palepale, nimerudi pale baada ya wiki moja mama mmoja akafa, na wengine wanaumwa, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa kunipigania.

DADA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA MTOTO WA JIRANI YAKE ALIYEKUFA KATIKA MAZINGIRA YA KUTANISHA AMERUDI BAADA YA MAMA YAKE KUJA KWA NABII FLORA NA KUOMBEWA


Bwana Yesu asifiwe; kwa kweli namshukuru Mungu wa Nabii Flora, jirani yangu alifiwa na mtoto wake, alikuja akiwa anaangaika, anasema anatafuta Kanisa ambalo litaweza kumrudisha mtoto wangu, alizunguka sana lakini hakupata mafanikio. Siku hiyo wakamleta kwangu usiku, nikamwambia twende kwa Nabii Flora anaweza mtoto wako atarudi. Nikawa nikija naye hapa ananiambia hivi kweli inawezekana, nikamwambia wewe amini tu, mimi ni Mwislamu lakini nimeamua kunga’ang’ania pale pana upako, kwa hiyo wewe kuwa na uaminifu ipo siku mtoto wako atarudi. Basi mtoto amesharudi, na anajiandaa kwa safari anataka kuja, tunamshukuru sana Mungu wa mahali hapa.

MWAJABU ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA UKIMWI, PIA AMEPANDISHWA CHEO KAZINI


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mwajabu; namshukuru Mungu wa madahabahu hii, nilikuwa na UKIMWI nimepona, pia nilikuwa mwalimu wa sekondari kwaida, lakini sasa hivi nimepandishwa cheo, nimekuwa academic , namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa kunitendea.


JINSI YA KUFIKA KANISANI
Kama unatokea Mwenge panda magari ya Tegeta, shuka Mbezi Mbuyuni,
uliza kanisani kwa Nabii Flora Peter.

Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com

No comments:

Post a Comment