DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Tuesday, February 25, 2014

WAIMBAJI 20 KUVAMIA JUKWAA MOJA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU MOJA YA MWIMBAJI MMOJA MESS JACOB CHENGULA JUMAPILI HII UBUNGO PLAZA

Sipati picha siku hiyo niyakapoona mastaa 20 wa nyimbo za injili wakihahakikisha AC za Ubungo Plaza hazifanyi kazi kwa kitimutimu kikali siku hiyo.


Sipati picha kuona Waziri wa Mawasiliano Mh Januari Makamba akicheza na kufurahia pale mzee mzima Mess Jacob Chengula atakapo shika kipaza sauti na kuvurumishi wimbo wa Mungu Habadiliki.
Sipati picha kuona blogger, Rulea Sanga atakapokuwa busy sana na kufotoa picha za watu ili mwisho wa siku kutnagaza matendo makuu ya Mungu kwa kupitia waimbaji.

Sipati picha siku hiyo kuona wachungaji na watumishi mbalimbali kusakata rumba la Yesu siku hiyo wakati mastaa wa nyimbo za Injili 20 watakapovamia jukwaa.

Kumbuka katika mkono wako shikilia mshiko wa kutosha kwaajili ya kujipatia DVD yako na Tshirt za Mess Jacob Chengula kwa bei nafuu kabisa.

Ndugu yangu na rafiki yangu usikose siku ya Jumapili 02/03/2014 saa 6:00 mchana baada ya ibada kujongea katika eneo hilo ukiwa umeshikilia 5,000 au 10,000 kwa viti vya VIP.
Mess Jacob Chengula

Tangazo limetengezwa na RumAfrica +255 715851523

Tembelea
www.messchengula.blogspot.com

No comments:

Post a Comment