DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Monday, March 17, 2014

FILAMU YA MAISHA YA NUHU YAPIGWA STOP NCHI ZA KIARABU


Filamu ya Hollywood iliyochukua bajeti kubwa sana ikiwa na jina la ‘Noah’ ambayo imeigizwa na Russell Crowe kama Nuhu imepigwa marufuku kuoneshwa katika nchi wanachama wa Umoja wa nchi/Falme za Kiarabu (United Arab Emirates).

Filamu hiyo imepigwa marufuku kwa madai kuwa kwanza inazua mtazamo tofauti kutokana na utofauti uliopo kati ya Biblia na Quran kuhusu simulizi la Nuhu na gharika ingawa kuna mfanano katika vitabu hivyo vitakatifu kuwa kulitokea mafuriko na Mungu akamwambia Nuhu ajenge safina.

Sababu ya pili ni kuonesha mfanano wa nabii na muigizaji wa kawaida hali inayoweza kuzua hisia tofauti kwa baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu.

Mkurugenzi wa maudhui ya vyombo vya habari wa umoja wa nchi/falme za Kiarabu (National Media Centre-United Arab Emirates), Juma Al-Leem, ameiambia Associated Press kuwa filamu hiyo haitaruhusiwa kwenye nchi hizo kwa kuwa inakinzana na miiko katika dini ya kiislam hasa katika kumfananisha nabii na mtu wa kawaida.

“Kuna vipande vya filamu hiyo ambavyo vinakanganya (simulizi) kati ya Biblia na Uislam, kwa hiyo tumeamua kuacha kuionesha.” Alisema Juma Al-Leem.

“Ni muhimu kuheshimu dini hizi mbili na kuacha kuonesha filamu hiyo. Taasisi ya kiislamu ya Al-Azhar ya Misri, imeeleza kuwa imeikataa filamu hiyo kwa kuwa iko kinyume na mafundisho ya dini hiyo na kwamba kuonekana kwa kukataa kuonesha taswira ya mtu ikifananishwa na ile ya nabii kutasaidia kuepuka watu kuanza kumuabudu mtu badala ya Mungu.

credits:Times fm

No comments:

Post a Comment