DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Sunday, April 20, 2014

DUNIA INA MAMBO:WAUMINI WADEKI BARABARA KWA SABUNI KUMLAKI NABII WAO HUKO KENYA


Ripota wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoitch anaripoti kwamba wakazi wa jiji la Eldoret wamemfanya kila alieiona hii kuvutiwa na pengine kujua imekuaje wakafanya hivi kwa mara ya kwanza baada ya kujitosa na kupiga deki barabara ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya.

Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya kumlaki nabii Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya leo na siku ya Jumatatu kuadhimisha pasaka na kumshukuru Jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret kufanyika uchaguzi wa amani mwaka 2013 Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii maoni yalikotolewa na Wakenya kuhusu hii ishu, maoni mengi yameonekana kupinga kitendo cha waumini hao wa kanisa la Jesus is lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima kupita kiasi. Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki Radio ya kass fm inayotangaza kwa lugha ya kikalenjin inayozungumzwa na wakazi wa jiji la Eldoret Julius lamaon, amesema ‘watu wetu waache kupotoka, jiji letu limebadilishwa na kuwa jiji la vituko…… Gavana hatakiwi kuhudhuria mkutano huu’

No comments:

Post a Comment