Hii
inaleta raha ndani ya mtima ninapoona vijana wanajituma kwa kazi ya
Mungu. Kwakweli binafsi nafarijika sana mpaka natamani na mimi Mungu
angenipa kipaji cha uimbaji ili niwe kama wao, lakini haiwezekani kwani
Mungu alinipa karama hii ya kubofywa bofywa kompyuta na kukuletea
habari zinazoendelea duniani hapo ulipo.
Mess Jacob Cjhengula baada ya kumtumikia Mungu katika mkutano wa MOROGORO YOTE KWA YESU unaoendelea katika mkoa wa Morogoro katika viwanja vya K/Ndege na Mtume Peter Nyaga wa kanisa la RGC akishirikiana na mwenyeji wake mwinjilis Jailos Maloda, leo hii amefunga safari kurudi Dar es Salaam tayari kwa kujianda na safari nyingine ya kuelekea nkoani Shinyanga na Mwanza katika tamasha la Pasaka ambapo kutakuwa na waimbaji wengi sana kama vile Rose Muhando, Sekeleti wa Zambia, Sarah K wa Kenya, Upendo Nkone na wengine wengi.
Mess Jacob Chengula akiwa mkoani Morogoro
Mess Jacob Chengula hakika ameamua kufanya kazi ya Bwana kwa mali zake na kutojali kupoteza muda wake wa kutafuta fedha, bali anaamini mali na fedha zatoka kwa Bwana. Tunachotakiwa ni kumuombea azidi kusonga mbele kwa kazi hii aliyoianza ya kumtumikia Mungu kwani kwa hiki anachofanya watu wanazidi kumpenda Mungu na kutoka rudi nyuma. Nyimbo zake ukisikiliza katika albamu yake ya MUNGU HABADILIKI utaamini kile naongea na wewe sasa. Kuna ujumbe mzuri sana wa kukuelimisha, kukuadibisha, kukufundisha na kukuburudisha.
Tumtakie afya njema ili azidi kuwaleta watu kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Wakristo tumekuwa na moyo wa kutowatia moyo watumishi wa Mungu wanavyofanya kazi ya Mungu, hii sio tabia nzuri kabisa. Tujaribu kuwa mfano wa kuwaunga watu wa Mungu wanavyofanya kazi ya Mungu na kutnga muda kuwaombea ili wanapofanya kazi ya Bwana wafanye kutokana na maagizo ya Mungu na sio akili zao. Kwa leo ninasema kwaheri
Wenu katika Bwana Rulea Sanga

kulia ni Joshua Makondeko akifuatiwa na Mess Jacob Chengula na Masanja Mkandamizaji
Mess Jaco Chengula akiwa na mama yake pembeni akiwa katika mkutano ulioandaliwa na Mchungaji Chacha wiki moja iliyopita mkoa Iringa
No comments:
Post a Comment