Si kitu
cha kawaida kuwakusanya watu wengi kiasi hiki kufika katika shughuli
yako. Lakini sisi tunayemtumainia Mungu si jambo la kushangaa kwani
tunatambua ni kitu tunafanya kwa utukufu wa Mungu. Waimbaji hawa
wameonyesha moyo wa AGAPE na wana hofu na kazi ya Mungu na ndio maana
wameona hakuna haja ya kutofika katika kumuunga mkono mtumishi wa Mungu
Mercy Charles Kitundu katika uzinduzi wa albamu yake ya "IMBENI SIFA ZA
YESU"
Ni
matumaini yetu, wewe unayesoma tangazo hili utafika katika tamasha hili
la kipekee lenye kibali cha Mungu. Waimbaji wamejipanga kuhakikisha
kazi ya Mungu inafanyika kwa kiwango cha juu. Uzinduzi huu utakuwa mfano
wa kuigwa kwani kutakuwa na vitu ambavyo havijafanyika katika matamasha
mengine.
Utaweza
kumsikia Mercy Kitundu aliyekuwa ameolewa na ndoa ya Kiislamu na baada
ya ndoa yake kuingia doa aliamua kuanza maisha mengine ya nje ya ndoa.
Hakukaa vizuri akapata janga lingine la kufiwa na wanawe wa pekee
wawili. Na sasa hana mume na hana watoto waliokuwa wakimfariji, ila
anasema anaye YESU MFARIJI ambaye aliwezaa kumpa kitu cha kumfariji
nacho ni kipaji cha UIMBAJI. Uimbaji umekuwa faraja kwake na sasa
anataka kuambukiza upako huu kwako wewe utakayefika siku hiyo.
Wewe
unayepitia mapito kama ya huyu mwimbaji usikose siku hiyo, Mungu
anaweza kuongea na wewe kwa njia ya uimbaji na ukatoka na jibu zuri na
kufarijika.
Tangazo limetengezwa na RumAfrica +255 715 851523
SIKILIZA NYIMBO MBILI ZA ZILIZOMO KATIKA ALBAMU YA IMBENI SIFA ZA YESU
No comments:
Post a Comment