Katibu Mwenezi wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania Stella Joel
akiongea na RUMAFRICA siku ya Jumatatu kuhusiana na tamasha
litakalofanyika mkoani Mbeya katika viwanja vya Nzovwe CCM kuanzia saa
6:00 mchana na baadae katika ukumbi wa Mtendwa Sunset siku ya tarehe 20
hadi 21 Juni 2014.
Rumafrica Online TV Logo
Kabla
ya yote aliweza kutoa historia fupi ya CHAMUITA kwamba ni chama
kilichoanza mwaka 2011 ambapo kilianza na watu wawili na baadaye watu
walianza kuongezeka na kuwa wengi sana, na sasa kimekuwa na kanda
mbalimbali kama vile Kanda ya kaskazini (Tanga, Arusha, kilimanjaro
Arusha na Manyara), kanda ya Morogoro na Pwani, kanda ya ziwa na huko
kote kuna viongozi. Pia alisema zoezi la kuhamasisha bado linaendelea na
ndio maana wameamua sasa kwenda mkoa wa MBEYA kuwaelimisha watu
kuhusiana faida za kuwa mwanachama wa CHAMUITA na kuwaunganisha
wanamuziki wa mkoa wa Mbeya pamoja
Katibu Mwenezi wa CHAMUITA, Stella Joel
Mkoa
wa Mbeya umebahatika na kuwa na chama chao cha muziki lakini bado
hakijasajiliwa, na hii ndiyo iliyowafanya viongozi wa CHAMUITA kwenda
kuwaeleza wanamuziki wa Injili kujiunga na CHAMUITA kwani ni chama
kilichosajiliwa na serikali na pia kujipatia haki zao kama waimbaji wa
nyimbo za injili Tanzania.
SIKILIZA STELLA JOEL AKIELEZA MENGI
JUU YA FAIDA ZA KUWA MWANACHAMA WA CHAMUITA NA PIA AKIELEZA JUU YA
MWANAMUZIKI ALISOMEWA KIFUNGO CHA MIEZI MITATU JELA.
BONYEZA HAPA KUMSIKILIZA STELLA JOEL
BONYEZA HAPA KUMSIKILIZA STELLA JOEL
Tangazo limetengezwa na Rumafrica +255 715 851523
No comments:
Post a Comment