Siku ya leo 15/06/2014 Mess Jacob Chengula alikuwa akimwimbia Mungu
katika mkutano wa Injili uliofanyika Ukonga Mazizini hapa jijini Dar es
Salaam katika kanisa la PEFA kwa mchungaji Jacob Elly.
Atosha Kissava (kulia) akienda sambamba na Mess Jacob Chengula (kushoto)
Mkutano
huu ulikkuwa wa kipekee kabisa kwani watu walionekana kubarikiwa na
uimbaji wa Mess Jacob Chengula hasa katika wimbo wake wa Mungu
Habadiliki. Katika mkutano huu kulikuwa na waimbaji mbalimbali kama Bony
Mwaitege, Atosha Kissava na wengine wengi.
Mess Jacob Chengula
Mess
Jacob Chnegula siku ya alhamisi anategemea kuelekea katika mkutano wa
Injili ulioandaliwa na Chama Cha Muziki Tanania (CHAMUITA) mkoani Mbeya.
Watu wa Mbeya wataenda kubarikiwa sana na mwimbaji huyu kwani kwa sasa
ametoa wimbo mpya unaoenda kwa jina la NANI KAMA YESU ambao unamguso wa
ajabu ukisikiliza na kufuatilia kile anaimba. Mwimbaji huyu ni kati ya
waimbaji wanaopenda sana kufanya kazi ya Mungu katika viwango vya
kimataifa. Hakika ukiangalia video yako utaamini kile ambacho
ninakisema.
Mess Jacob Chengula
Kwa
wasiomjua Mess Jacob Chengula ni mwimbaoji wa nyimbo za Injili ambaye
anatokea katika mkoa wa Iringa-Makete. Kabla hajaanza kazi ya Mungu
alikuwa mwanamuziki wa Bongo Flava na alikuwa mtaalamu wa kuazimisha
vifaa vya muziki akiwa Makambako Iringa.
Kulia ni Bony Mwaitege akiwa na Mess jacob Chengula
Elimu
yake ni darasa la saba lakini Mungu amemuinua na sasa ni mfanyabiashara
mkubwa Kariakoo jijini Dar es Salaam, ameoa na ana watoto. Mess alianza
biashara akiwa kijana mdogo sana (akiwa na miaka 16) ambapo alifanikiwa
kuwa moja wa wafanyabiashara wakubwa mkoani kabla hajaokoka.
Baadaye
alifilisikia kabisa ndipo alipoona msaada uko kwa Yesu Kristo. Mess
Jacob Cohengula aliamua kuokoka na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
Rumafrica ipo katika maandalizi ya kumtafuta mwimbaji huyu ili uweza kujua maisha yake na mipango yake ya baadae.
ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBONYZA (Read More) HAPO CHINI
No comments:
Post a Comment