Baada ya kazi nzito mkoani Mbeya katika Mbeya Gospel Festival, Emaanuel
Mabisa na Mess Jacob Chengula waliweza kumtangaza Yesu Kristo kwa njia
ya uimbaji katika Camp ya vijana wa Pentekostal Holiness iliyofanyika
katika chuo cha Kileluu mkoani Iringa.
Mess Jacob Chengula
Hii inapendeza sana kuona vijana wanaacha kazi zao na kupoteza muda kwa kazi ya Mungu. Vijana wengi tuko busy sana kwa kazi za duniani na tunatumia muda mdogo sana kwa kazi ya Mungu. Tunapokuwa na shida tunamtafuta sana Mungu lakini tukiwa katika starehe tunamsahau Mungu Baba. Mess Jacob Chengula na Emmanuel Mabisa wameliona hilo na ndio maana wameamua kumtumikia Mungu wakati wa ujana wao.
Emmanuel Mabisa
Tukumbuke siku ya mwisho Mungu wetu atatuuliza tulifanya nini wakati tupo duniani, tutatoa hesabu zetu. Hujachelewa kijana mwenzangu, amua sasa kufanya kazi ya Mungu kama punda kwa kuhubiri injili ya Yesu Kristo na kuwaleta watu kwa Yesu Kristo. Tuache kujiona mastaa na kuionea aibu injili ya Yesu.
Kila mtu hapa duniani amepewa kazi ya kufanya kwaajili ya utukufu wa Mungu. Muulize Mungu wako nini cha kufanya kwaajili yake naye atakujibu na kukupa kazi ya kufanya. Nadhani unajua ya kwamba kama hutafanya kazi ya Mungu na ukaamua kumtumikia shetani, basi siku ile ya mwisho utatupwa jehanamu ukiungua kwa moto mkali sana.
Watumishi wa Mungu hubiri injili ya kuwapeleka watu kwa Mungu, na tuache kuhubiri ili watu wajae kanisani na tupate sadaka nyingi. Huu ni wakati wa kumtumikia Mungu wetu. Watumishi wa Mungu fikeni vijijini kwani huko watu wanateseka sana na wanakosa watu wa kuwainua kiimani. Wamezungukwa na mapepo, majini, wachawi na wamekuwa wafungwa wa kiroho
Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS

No comments:
Post a Comment