Kanisa la Tanzania Assemblies Of God linatazamia kutimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake katika nchi ya Tanzania. Kanisa hilo ambalo kihistoria lilianza mwaka 1939 linatazamia kufanya kilele cha Jubilee hiyo katika mwezi wa July katika Mkoa Wa Mbeya.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Kanisa hilo la TAG lilizindua rasmi mbio za shughuli mbalimbali za Kanisa hilo zitakazokuwa zikifanywa ili kuelekea Kilele Cha maadhimisho hayo. Siku Ya Jumamosi katika Kanisa lililo Mbalizi Mkoani Mbeya ambako ndiko inakosaidikika kuwa Kanisa hilo lilianzia ulifanyika Uzinduzi wa Kanisa hilo ambalo limejengwa Upya kama sehemu ya maadhimisho ya kusheherekea miaka 75. Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dr. Barnabas Mtokambali alieleza kuwa kuanzia siku hiyo Program Mbalimbali zitakuwa zikifanyika kama sehemu ya maadhimisho ya miaka hiyo 75. Akifafanua alieleza kuwa katikati ya mwezi wa 4 na 6 mwaka huu Idara zote zilizo chini ya Kanisa zitaendesha Program Maalum kama sehemu ya maashimisho lakini Pia Majimbo yote yaliyo chini ya Kanisa hilo wataendesha Program Maalum kama sehemu ya Maadhimisho hayo.
Kanisa hilo lenye Slogan ya "Miaka 10 Ya Mavuno, Tanzania Kwa Yesu" linatazamia kutimiza miaka 75 likiwa limeongozwa na maaskofu Wakuu watatu Mpaka sasa, Dr. Emmanuel Lazaro aliyeongoza kwa miaka 26, Dr.Ranwel Mwenisongole aliyeongoza kwa miaka 16 na sasa Kanisa linaongozwa na Dr. Barnabas Mtokambali ambaye amekaa 6 mpaka sasa. Mfumo huu wa Kiongozi ulianza kutumika rasmi Kanisa hilo lilipoanza kujiendesha Kama Taasisi rasmi.
Kamati
Kuu pamoja na Wamishenari wa Kanisa hilo wakishirikiana kuzindua
Program mbalimbali za kanisa hilo walipokuwa Mbalizi Mkoani Mbeya. Picha na habari SAMSASALI.BLOG |
No comments:
Post a Comment