DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Wednesday, January 22, 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA ELIZABETH NGAIZA ASIMULIA YALIYOMKUTA BAR KABLA YA KUOKOKA


Mungu huwatoa mbali watu, huwatoa katika mashimo marefu sana, huwatoa watu katika moto mkali sana, huwatoa watu katika shida mbalimbali, huwatoa watu katika magonjwa sugu na sehemu mbalimbali walizofungwa na adui shetani na kuwatumikisha kama watumwa. Mungu wetu ni Mungu wa huruma na upendo.

Elizabeth Ngaiza katika ofisi ya Rumafrika

Elizabeth Ngaiza ni mwimbaji nyimbo za Injili Tanzania. Anamtumikia Mungu kwa mali zake na akili zake kufikisha ujumbe wa Mungu kwa wale wenye uhitaji wa kumjua huyu Mungu wetu na Baba yetu kwa njia ya uimbaji. Hakika Mungu anamtumia ipasavyo, na hii ni kutokana na ujumbe ambao hutoa pale tu anapopata nafasi ya kufanya kazi ya Mungu kwa kutumia karama yake ya uimbaji. Kama umewahi kusikia nyimbo zake utaamini ya kuwa Mungu wetu ni Mungu anayetumia watu wake kupeleka ujumbe kwa watu wote kwa kutumia njia mbalimbali.

Elizabeth Ngaiza akiongea na RumAfrica aliweza kufunguka na kuelezea maisha yake kabla ya wokovu. Elizabeth Ngaiza alisema kabla hajaokoka alikuwa ni mtu wa kushinda bar akinywa pombe  mpaka inafika point analewa kabisa. Maisha yake yalikuwa hayampendezi Mungu kabisa, ilifika kipindi akawa anafanya mashindano na mume wake kwa kushinda bar akipiga pombe.

Muda wake wa kurudi nyumbani ni usiku wa manane. Siku zingine akiona mume wake amerudi usiku wa manane, na yeye siku ya pili atahakikisha anarudi usiku wa manane kwa lengo la kumkomoa mume wake.

Elizabeth Ngaiza ni Muhaya kwa kabila, alisema siku zingine akiwa hana pesa ya kununua bia, alikuwa anajitahidi kutafuta pesa hata kwa kukopa ili mradi ashinde bar akinywa pombe. Siku zingine akikosa pesa atajitahidi hata kutafuta hata kiasi kidogo anunue hata soda, ili mradi akae bar na arudi usiku.

Hali hii ilimtesa sana Elizabeth Ngaiza  kwa muda mrefu sana. Sheatani alimtumikisha sana na kumuabisha katika jamii inayomzunguka na ndugu zake.

Ushuhuda unaendelea. Utaweza kujua mume wake alikuwa anamchukuliaje kama mke wake?
Familia yake ilikuwa akimchukuliaje?
Maisha yake kiujumla yalikuwaje?

Ni kitu gani kilimfanya aokoke?

Kwa siku leo tutaishi hapa.
Unaweza kuwasiliana na Elizabeth Ngaiza kwa simu +255 714294076

MUNGU WANGU AKUBALIKI SANA

No comments:

Post a Comment