Bwana Yesu asifiwe; mara ya kwanza nilimuona Nabii Flora nikiwa Swaziland masomoni kwenye mtandao, nakumbuka ilikuwa mwaka 2012 mwishoni. Kabla ya kwenda masomini nilikuja kumuona Nabii Flora, kwa hiyo aliniombea maji ilikuwa ni mwaka wangu wa mwisho.
Nilipokuja hapa kukaa tu akaniambia nakuona kama unapanda kwenye ngazi, utakuja kupata kitu kikubwa sana maishani. Mimi sikuelewa kwa sababu kulikuwa na safari ya kwenda Uingereza katika shule yetu lakini ilikuwa ni vigumu sana kupata. Basi ikaenda mwezi wa kwanza nikaambiwa nimekosa hiyo safari, kwa hiyo bado nikawa nashindwa kuelewa Nabii alikuwa anamaanisha nini. Mimi nilikuwa ni mtundu wa Computer, likatokea shindano lililozaminiwa na umoja wa mataifa, wakasema kwamba wanatafuta dunia nzima vijana ambao niwabunifu kwa mambo ya Computer.
Basi mimi na rafiki yangu tukaomba lakini ilikuwa kushinda kwetu ni vigumu kwa sababu tulikuwa hatuna hata diploma, lakini ilipofika mwezi wa kumi tukaambiwa kwamba sisi ni moja ya washindi kumi kati ya watu mia sita kutoka nchi 88 dunia nzima.
Cha ajabu ni kwamba toka ilo shindano lianze hakuna mtu ambaye yupo kwenye A-level hakuna ambaye ameweza kushinda ilo shindano, na sisi ndio tulikuwa ni watu wa pekee ambao hatuna hata Certificate. Kwa hiyo katika hiyo nafasi tuliyoipata, wametupa milioni 8 ya kuanzisha hiyo Kampuni na kuuza hizo bidhaa ambazo wamezitengeneza, na mpaka sasa hivi hiyo kampuni imeshasajiliwa ipo Swaziland, na Mungu akipenda nitaenda huko mwezi wa pili kuzindua. Na kwa watu ambao wapo kwenye mtandao wanaweza wakaangalia hilo shindano.
Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com
JINSI YA KUFIKA KANISANI
Kama unatokea Mwenge jijini Dar, panda magari ya Tegeta shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni na uliza kanisa la Nabii Flora Peter.
No comments:
Post a Comment