Mungu huwatoa mbali watu, huwatoa katika mashimo marefu sana, huwatoa watu katika moto mkali sana, huwatoa watu katika shida mbalimbali, huwatoa watu katika magonjwa sugu na sehemu mbalimbali walizofungwa na adui shetani na kuwatumikisha kama watumwa. Mungu wetu ni Mungu wa huruma na upendo.
Elizabeth Ngaiza katika ofisi ya Rumafrika
Elizabeth Ngaiza ni mwimbaji maarufu sana wa nyimbo za Injili Tanzania. Anamtumikia Mungu kwa mali zake na akili zake kufikisha ujumbe aliopewa na Mungu kwa njia ya uimbaji. Mungu amekuwakuwa mwaminifu kwake na anamtumia iapasavyo. Kama umewahi kusikia nyimbo zake utaamini kuwa Mungu wetu ni huruma na hujibu maswali ya walio wengi.
Elizabeth Ngaiza akiongea na RumAfrica aliweza kufunguka na kuelezea maisha yake kabla ya wokovu. Elizabeth Ngaiza alisema kabla hajaokoka alikuwa ni mtu wa kushinda bar akinywa pombe sana. Maisha yake yalikuwa ya ovyo sana, ilifika kipindi akawa anashindana na mume wake kunywa pombe bar na kurudi usiku wa manane akiwa amepombeka sana nap engine kutojitambua. Alikuwa akifanya haya yote kwa lengo la kushindana na mume wake, kwani mume wake naye alikuwa ni mtu wa kushinda bar na kurudi usiku wa maneno.
Elizabeth Ngaiza ni Muhaya kwa kabila, alisema siku zingine akiwa hana pesa ya kununua bia, alikuwa anajitahidi kupata hata pesa ya soda ili mradi akae bar kwa muda mwingi na arudi nyumbani usiku wa manane kwa kumkomoa mume wake. Hali hii ilimtesa sana Elizabeth Ngaiza kwa alikuwa akiishi maisha ya kuteswa na mwovu shetani. Hakika shetani alimtumikisha Elizabeth Nagiza kwa muda mrefu sana, akiongea na Rumafrica huku akiwa na huzuni moyoni mwake.
Kwa siku leo tutaishi hapa, ushuhuda ohuu unaendelea zidi kutembelea blogu hii utajua mengi na ni kitu gani kilimfanya aokoke na kuwa mwimbaji.
Unaweza kuwasiliana na Elizabeth Ngaiza kwa simu +255 714294076
MUNGU WANGU AKUBALIKI SANA

No comments:
Post a Comment