Baada ya Lord Eyes kukamatwa kwa tuhuma za wizi, msanii wa kizazi kipya aliyekuwa mpenzi wake Ray C afunguka na kumuomba msanii huyo kubadilika, na huu ndio ujumbe aliouandika muda mchache kupitia account yake ya Instagram
Mimi kama Rulea Sanga ninasema huu ni mtihani tulioachiwa sisi tunaejiita tumeokoka na tuko duniani kuokoa waliopotea. Huyu ndugu yetu ni maarufu sana nchini Tanzani na ni mwimbaji mzuri sana katika muziki wa kidunia, lakini mambo anayofanya ni ya kijinga sana ambayo hata mtoto mdogo hawezi fanya. Tangia nianze kusikiliza musiki na kuwajua wanamziki sijawahi kusikia vituko kama vya huyu ndugu yetu.
Kama Mkristo nini unaweza kukufanya kwa huyu ndugu yetu ambaye Mungu ampa kipaja cha uimbaji na nyota ya kupendwa na wengi. Unaonaje wewe ukawa mfano mkubwa wa kumwendea huyu jamaa na kumueleza habari za Yesu Kristo na kuhakikisha anaokoka na kumwimba Mungu. Nina uhakika Mungu atakubaliki sana na Taifa la Tanzania litakupongeza sana kwa juhudi zako.
kulia ni Lordeyez
Kumbuka huyu jamaa ndiye aliyempoteza dada yetu Ray C ambaye alikuwa mtangazaji wa Clouds FM na baadae kuwa mwanamuziki. Ray C alidanganyika na kuamua kuwa mpenzi wake. Jamaa mbali na mapenzi akaanza kuvutisha sigara na baadae bangi na mwisho wa siku madawa ya kulenvya ambayo yaliharibu future ya dada yetu Ray C na kuwa kama chizi mtaani. Tunamshukuru Rais Kikwete kwa juhudi zake za kumuweka sawa Ray C na mpaka sasa amepona kabisa na amekuwa balozi kwa watumiaji madawa ya kulevya.
Kingine nataka kusema ni kwamba Lordeyez pengine sio yeye anafanya ila ni nguvu tu za giza zimemzunguka na zinamsukuma kufanya mambo ya kijinga. pengine kalogwa na jamaa zake kutokana na uimbaji wake mzuri au kafanyiziwa. Nakumbuka mwaka jana alikubwa na balaa hilo la kukamatwa akiiba site mirror za mwimbaji mwenzake Dimpoz na alipokamatwa alikiri kuwa ni kweli alifanya hilo tukio na Dimpoz alimsamehe... Baada ya kusamehewa Lordeyez alikiri kutofanya tena.
Kinachonishangaza ni jina lake la kisanii, anajiita Macho ya Mungu (Lord Eyes) halafu anakuwa jambazi na mtumiaji wa madawa ya kulevya. Huyu jamaa inaonekana alipokuwa anajiita jina hilo alikuwa na hofu ya Mungu au alikuwa anampenda Mungu na ndiyo maana aliamua kuacha majina mengine na kuamua kutumia hilo. Lakini sasa shetani anamtumia kisawasawa kuhakikisha dreams zake ninakwishna..Poa jamani tumsaidie ndugu yetu kwa maomabi na sala.
Ninamaliza kwa kusema, hebu jitose na ongea na huyu mtu aachane na tabia ya wizi na mwisho wa siku mlete kwa Yesu Kristo. Ninasema ukifanikiwa utaona mwenyewe Mungu atakavyofanya miujiza katika maisha yako. Na mimi ninajitahidi na ninaamini ipo siku Mungu atanigonganisha na huyu jamaa na nitamleta kwa BWANA....Mungu wangu na akubaliki na akupe ujasiri wa kuongea na Bwana Lordeyez
Wenu katika Bwana
Rulea Sanga. Mkinga kutoka Ugabwa Makete
No comments:
Post a Comment