DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Thursday, March 6, 2014

SEHEMU YA TANO: TAMASHA LA UZINDUZI WA ALBAMU YA MESS JACOB CHENGULA YA "MUNGU HABADILIKI" SIKU YA JUMAPILI 02.03.2013 -UBUNGO PLAZA DAR ES SALAAM

Jamani tumeshuhudia matamasha mengi sana lakini hili la Jumapili lilikuwa la tofauti sana. Katika matamsha yaliyoongoza kuwa na waimbaji maarufu nchini Tanzania wanaomwimbia Mungu hili la Jumapili ni la kwanza, hatujui huko baadae. Waimbaji kukusanyika kwa pamoja zaidi ya 20 na kumwimbia Mungu si jambo rahisi. Hii ni kwa Neema tu ya Mungu. Mess jacob alikonga mioyo ya watu kwa ubunifu wake na juhudi zake za kuhakikisha waimbaji wote aliotarajia kufika wamefika, hata kama kuna baadhi hakuonekana lakini hakuna kasoro iliyotokea kwa mashabiki wa mambo ya Mungu.

Tamasha hili lilifanyika katoika ukumbi wa Ubungo Plaza na mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Mawasiliano Mh. Januari Makamba akiongozana na familia yake na baadhi ya watumishi wa Mungu kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa.
Katika tamasha hili kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao, mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite. 
Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi. 
Mgeni rasmi Januari Makamba alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji. Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika huduma yao ya uimbaji.
Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao. Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.


Malikia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando akifanya yake kwa utukufu wa Mungu


Rose Muhando akihakikisha kazi ya Bwana inasonga kwa uimbaji




Dancers wa Rose Muhando wakicheza style ya Makirikiri

Rose Muhando
Dancers wa Rose Muhando

Mke wa Mh Januari Makamba aliyeshika mkono mwanae akielekea stejini kumtunza Rose Muhando
Mama Januari Makamba na mwanae (kushoto) wakielekea katika kiti chao baada ya kumtunza Rose Muhando stejini

Edson Mwasabwite akiimba wimbo wake wa Ni kwa Neema tu

Edson Mwasabwite akipaza sauti kwa Bwana kwa kumuimbia
Kutoka kulia ni Atosha Kissava, Beatrice Mwaipaja, Neema Gasper na Tumaini Njole


Mh. Januari Makamba akiwaaga waimbaji wa nyimbo za injili mara baada ya kumaliza zoezi la uzinduzi wa albamu ya Mess Jacob Chengula. Hapa anasalimina na Mwinjilisti Sarah Mvungi ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili na ni daktari
Madam Ruti akiimba wimbo wake wa jana imepita
Madam Ruti akiimba wimbo wake wa jana imepita, watu wakiselebuka kwa Yesu

Madam Ruti akiimba wimbo wake wa jana imepita huku watu wakipokea baraka zao na mioyo yao kufarikika na kufurahi


Upendo Nkone akienda sawa kwa utukufu wa Mungu
Hata sasa vidole juu..Upendo Nkone kiboko, Mungu anamtumia ipasavyo kwa uimbaji

Faraja Ntaboba kutoka nchi ya Congo siku hii aliimba wimbo wa Yuko Mungu
Faraja Ntaboba akihakikisha anatumia fursa aliyopewa na Mungu ya uimbaji kisawasawa
Haya sasa,,,mzee mwenyewe, Mess Jacob Chengula akimtukuza Mungu na kumsifu kwa jinsi alivyomfanikisha kutimiza ndoto yake ya kuzindua albamu yake ya Mungu Habadiliki
Dancers wa Mess Jacob Chengula wakifanya yao kwa utukufu wa Mungu
Tumaini Njole



MESS JACOB AKIFUNGA TAMASHA LAKE KWA UIMBAJI NA KUWASHUKURU WALE WOTE WALIOFIKA KUMUUNGA MKONO


























Picha zimepigwa na RumAfrica
Tembelea
+255 715 851523
POSTER NA TIKETI NI KAZI YA RUMAFRICA. TUNAKUKARIBISHA


No comments:

Post a Comment