Jamani tumeshuhudia matamasha mengi sana lakini hili la Jumapili lilikuwa la tofauti sana. Katika matamsha yaliyoongoza kuwa na waimbaji maarufu nchini Tanzania wanaomwimbia Mungu hili la Jumapili ni la kwanza, hatujui huko baadae. Waimbaji kukusanyika kwa pamoja zaidi ya 20 na kumwimbia Mungu si jambo rahisi. Hii ni kwa Neema tu ya Mungu. Mess jacob alikonga mioyo ya watu kwa ubunifu wake na juhudi zake za kuhakikisha waimbaji wote aliotarajia kufika wamefika, hata kama kuna baadhi hakuonekana lakini hakuna kasoro iliyotokea kwa mashabiki wa mambo ya Mungu.
Tamasha hili lilifanyika katoika ukumbi wa Ubungo Plaza na mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Mawasiliano Mh. Januari Makamba akiongozana na familia yake na baadhi ya watumishi wa Mungu kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa.
Tamasha hili lilifanyika katoika ukumbi wa Ubungo Plaza na mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Mawasiliano Mh. Januari Makamba akiongozana na familia yake na baadhi ya watumishi wa Mungu kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa.
Katika tamasha hili kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha
juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya
waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao,
mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite.
Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni
rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa
la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa
lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi.
Mgeni rasmi Januari Makamba
alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji.
Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga
mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki
Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa
nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha
Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika
huduma yao ya uimbaji.
Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya
waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina
baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka
watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na
kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao.
Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi
kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza
kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika
masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili
yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.
Mess Jacob (kulia) akiwa na Rose Muhando wakati wa kuelekea stejini kwa kazi ya Bwana
Mess Jacob Chengula akijiandaa kuelea stejini
Mess Jacob Chengula akijiandaa kuelea stejini
Mess Jacob Chengula akijiandaa kuelea stejini
Kiongozi wa Chama Cha Muziki Tanzania na ni mwimbaji wa nyimbo za Injili John Shabani akiwa ameshika risala ya kumsomea mgeni rasmi
Rose Muhando kablayahajapanda jukwaa, akicheki upepo unaendaje...
Dancers wa Mess Jacob Chengula wakiwa stejini wakivuta vumbi kabla muhusika mwenyewe Mess Jacob Chengula hajapanda jukwaani
Mtangazaji wa Clouds FM na mwigizaji wa filamu Tanzania Uncle Jimmy wa www.unclejimmytemu.blogspot.com akifotoa mafotoz kwaajili yako wewe
Mtangazaji wa Clouds FM na mwigizaji wa filamu Tanzania Uncle Jimmy wa www.unclejimmytemu.blogspot.com akiwa amepooooziii baada ya kufanya yake
Mess Jacob akilivamia Jukwaa kwa wimbo wake wa MUNGU HABADILIKI
MessJacob Chengula akipaza sauti ya Bwana kwa nji ya uimbaji na kuwafata mashabiki wake waliko kwa utukufu wa Mungu
Watu hawaamini kinachoendelea kwa mwimbaji huyu Mess Jacob Chengula kufanya makubwa ukumbini
Mess Jacob Chengula akifanya yake katika siku hiii ya kipekee kwake
Mess Jacob Chengula
Wa pili kutoka kushoto ni mke wa Mh Januari Makamba akienda stejini kumtunza Mess Jacob Chengula
Wa pili kutoka kusho ni mwambaji wa nyimbo za injili Madam Ruti akifuatiwa na mtangazaji wa Praise Power Christina Mtua
Mh. Januari Makamba (wa pili kutoka kushoto) akielekea stejini kwaajili ya zoezi la kuzindua albamu ya MUNGU HABADILIKI ya Mess Jacob Chengula na nyuma yake ni mzee wa kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa
DVD za Mungu habadili zikipelekwa kwa Mgeni rasmi
MC Rita Chiwalo akitokelezea na Mh. Januari Makamba mara baada ya kufika stejini kwa kazi ya Bwana
Mess Jacob Chengula akipeleka DVD kwa mgeni rasmi Mh. Januari Makamba kwa kuzinduliwa
Mzee wa kanisa la Mito ya Baraka akiziombea DVD kabla ya mgeni rasmi kuzizindua
Mh Januari Makamba akifungua box la DVD za Mungu Habadiliki
Mh Januari Makamba akiwa tayari amezindua albamu ya Mungu Habadiliki. Hapa akiwaonyesha watu waliohudhuria siku hiyo kuwa imezinduliwa rasmi
Mh. Januari Makamba akimpongeza Mess jacob Chengula kwa hatua aliyofikia na akikipongeza Chama cha Muziki wa Tanzania pamoja na viongozi wake
Mgeni rasmi Mh. Janauri Makamba akiwa na Mess Jacob Chengula, MC Bony (kulia), Masanja Mkandamizaji (kushoto) na baadhi ya dancers wa Mess Jacob Chengula
Masanja akiwakaribisha watu katika zoezi la kumchangi Mess Jacob Chengula
USIKOSE KUANGALIA SEHEMU YA TANO YA MFULULIZO WA MATUKIO HAYA KWA KUPITIA BLOGU HII NA BLOGU YA RUMAFRICA
Picha zimepigwa na RumAfrica
Tembelea
www.rumaafrica.blogspot.com
+255 715 851523
POSTER NA TIKETI NI KAZI YA RUMAFRICA. TUNAKUKARIBISHA
No comments:
Post a Comment