ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas
Mtokambali amewaongoza wachungaji zaidi ya 800 kuchangia damu.
Askofu alisema uchangiaji damu huo ni moja ya adhima ya kanisa ili
kukabiliana na upungufu wa damu unaokikabili kituo cha damu salama kanda
ya Nyanda za juu kusini hivyo litaendeshwa kwa muda wa siku tatu
kuanzia Julai 10 hadi 12,mwaka huu ili kukamilisha wachungaji zaidi ya
1000 nchi nzima.
Alisema kama kanisa na Viongozi
wameguswa na tatizo la upungufu wa damu katika mahospitali kutokana na
watu kupata ajali kila siku, wanawake kupoteza damu nyingi wakati wa
kujifungua pamoja na watoto ndiyo maana wakaona ni vema wakaonesha mfano
wa kuchangia damu.
Aidha alitoa wito kwa viongozi
wengine wa dini bila kujali itikadi zao kuchangia damu popote pale
walipo ili kuokoa maisha ya Watanzania wenye mahitaji kwa kuwa damu
haiuzwi na hakuna kiwanda cha kuzalisha zaidi ya mtu kujitolea.
Kwa
upande wake Afisa tabibu wa Damu Salama kanda ya Nyanda za juu kusini
yenye makao makuu katika Hospitali ya Wazazi Meta jijini Mbeya, Alex
Kasimba,alisema ni kweli kuna upungufu mkubwa wa damu katika Benki yao.
Alisema
kwa takwimu za Mwaka jana damu iliyokuwa ikihitajika ni chupa 28000
lakini Benki ilifanikiwa kukusanya chupa 19000 sawa na asilimia 68 hivyo
kuwa na upungufu wa chupa 9000 sawa na asilimia 32.
Alisema
hata mwaka huu wanauhitaji wa kiasi kama hicho ili kuweza kuziba pengo
la upungufu wa damu ambapo kupitia maadhimisho ya Miaka 75 ya TAG
wanatarajia kukusanya zaidi ya Lita 400.
Aliongeza
kuwa taasisi za kidini kama TAG, Sabato, Waislam na taasisi za elimu
kama Shule za sekondari na vyuo ndiyo wanaojitolea kwa wingi damu
tofauti na wananchi wa kawaida.
ASKOFU mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali akichangia Damu
Baadhi ya wachungaji wa kanisa la TAG wakitoa damu na wengine wakisubiri zamu yao
ASKOFU mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali akipimwa Damu
Makamu Askofu Mkuu, Dk. Mhiche akipimwa damu kabla ya kutoa
Baadhi ya wachungaji wengine wakiwa katika foleni ya kujiandikisha kutoa Damu
ASKOFU mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas akiongea na waandishi wa habari
Afisa tabibu wa Damu Salama kanda ya Nyanda za juu kusini yenye makao
makuu katika Hospitali ya Wazazi Meta jijini Mbeya, Alex Kasimba
akiongea na waandishi wa habari
Anthony Damas mwandishi wa apostledarmacy.blogspot.com
Zoezi hilo liefanyika katika Chuo cha Biblia kilichopo Itende jijini
Mbeya ambapo Askofu huyo katika kuonesha uzinduzi na yeye alichangia.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchangia, alisema
Wachungaji wameona wachangie damu kutokana na upungufu na mahitaji
yanayoikabili Benki ya damu salama.
Alisema katika zoezi hilo ni wachungaji 800 ambao ni waangalizi wa
kanisa ndiyo watakaoanza kuchangia na kufuatiwa na wachungaji wote
kutona nchi nzima ambao watakuwepo mkoani Mbeya kwenye maadhimisho ya
miaka 75 ya TAG.
No comments:
Post a Comment