
Mzee
wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa kwa jina
la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya kukurupushwa
kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka kuvunja amri ya
sita na binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Debora
Jacob, Ijumaa lina kisanga cha aina yake.
Mzee wa kanisa la kiroho aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa,
HABARI KAMILI
Tukio
hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu maishani mwake, lilijiri
kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Segerea,
Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa
ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.
Katika tukio hilo, mzee
huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la Maigizo la Vivif lenye maskani
yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia kwenye gesti hiyo katika chumba
ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya kuchomolewa na
kufikishwa kanisani kisha polisi.
TUHUMA NZITO
Timu
ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, ikiwa kwenye
mingo zake, ilipokea simu kutoka kwa dada aliyejitambulisha kwa jina
moja la Diana na kujieleza kuwa anatoka kundi la sanaa za maigizo la
Vivif lililopo Segerea jijini Dar.
OFM: Ndiyo hujakosea unazungumza na
OFM, tukusaidie nini?
Diana:
Kuna mzee wa kanisa la kiroho la (anataja jina la kanisa hilo) lililopo
maeneo ya Segerea, aliomba kuwa mfadhili wa kundi letu.
Akiwa kwenye geti la kanisa.
Tulimkubalia na baada ya muda alianza kutumia fedha zake vibaya kwa kufanya vitendo visivyofaa.
OFM: Vitendo gani visivyofaa?
Diana: Anawarubuni mabinti wadogo anawaweka kambini na kula nao tunda tamtam eti ndiyo tiketi ya kuchezeshwa kwenye maigizo.
OFM: Tiririka!
Diana:
Yaani hadi muda huu ninapozungumza na ninyi mzee huyo wa kanisa
anachati na msanii mwingine wa kundi hilo. Anaitwa Debora anataka waende
kwenye gesti fulani wakanogeshane, wahini tayari mtego umewekwa
utafyatuka muda wowote.
UDHALILISHWAJI?
Diana
alisema baada ya Debora kuombwa ‘mambo’ ndipo akawataarifu wasanii
wenzake na kuwataka wote kwa pamoja waungane kuikomesha tabia hiyo chafu
ya Luca anayelichafua kanisa la kiroho na kulidhalilisha kundi lao la
sanaa.
OFM MZIGONI
Baada ya kuseti kila kitu,
Diana aliiomba OFM iambatane nao kwani muda huo tayari Debora
alishatangulia kwenye gesti hiyo kumfuata mzee huyo wa kanisa ambaye
alishachukua chumba.
.....akitaitiwa.
Taarifa
hiyo ilipokelewa kwa mikono miwili na kiongozi wa OFM ambaye aliwaagiza
vijana wake makini ambao walisitisha kazi nyingine za kiintelijensia
kisha kuelekeza nguvu zao eneo la tukio.
Vijana hao walitumia
pikipiki zao ziendazo kasi ambapo baada ya muda usiozidi dakika ishirini
walikuwa wamefika kwenye gesti hiyo.
ENEO LA TUKIO
OFM
walipofika eneo la tukio, walikuta kundi la wasanii hao wakimchomoa
gesti mzee huyo wa kanisa ambaye aliruka ukuta na kudondokea kwenye
matuta ya viazi.
Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la
wasanii hao lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye
chumba cha nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata
hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye
nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.
Baada
ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa kuwa
wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu
wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.
KABANG!
Alipotiwa
mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa
mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na
kuomba ushauri.
APELEKWA MSOBEMSOBE KANISANI
Kundi
hilo la wasanii lilimpeleka kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua
kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii
waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.
Mtuhumiwa akitembezwa mtaani.
MTAANI WERAAA!
Wakiwa
mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku
wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.
Wakiwa
kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na
waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
BREKI YA KWANZA POLISI
Kundi
la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa
wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya
vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha
Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba
RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA
WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.
Hadi OFM wanaanua jamvi kituoni hapo kanisa lilikuwa likihaha kumchomoa kwa dhamana akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Source:
Vituko vya mtaa