DVD YA MUNGU HABADILIKI YA MESS JACOB CHENGULA

Friday, May 1, 2015

PICHA:MESS JACOB CHENGULA AKIFANYA KWELI SIKU YA JANA TABATA KIMANGA.

 Mess Jacob Chengula akiwa na Rose Muhando katika Mkutano Mkubwa ulio andaliwa Tabata Kimanga na Mtume Peter Nyaga.
Muimbaji Mess Jacob chengula ameendelea kupata kibali kwa watanzania hii

Thursday, April 23, 2015

Wednesday, April 22, 2015

HAPA NIMEKUWEKEA PICHA ZA MATUKIO YA STAR MESS JACOB KATIKA TUA ZAKE MIKOANI.

Bwana anazidi kumuinua mtumishi wake Mess Jacob....wiki hii utakua ukipata matukio ya safari zake kutoka kwenye mikutano mbalimbali aliyo

Monday, April 20, 2015

EXCLUSIVE:AUDIO MESS CHENGULA ft UPENDO NKONE-MOYO HAUNA WOGA

Mess Jacob katika ubora wake.Chukua time yako kusikiliza brand new single kutoka kwa mkali MESS JACOB.....-MOYO HAUNA WOGA ft UPENDO NKONE.

Thursday, September 11, 2014

MATOKEO YA UZINDUZI WA ALBAMU YA MESS JACOB CHENGULA NA FAINALI ZA KOMBE LA MESS CUP MKOANI IRINGA


Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Mess Jacob Chengula mkazi wa jijini Dar es Salaam hivi karibuni alizindua albamu yake ya MUNGU HABADILIKI  mkoani Iring. Uzinduzi huu uliambatana finali za mpira wa miguu, wachezaji walikuwa wakiwania kombe la MESS CUP lililoandaliwa na mwimbaji huyu.

Tamasha hili lilihudhuriwa na watu wengi sana ambao walitamani kumuona Mess Jacob Chengula akimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Watu walibarikiwa sana na kile kilichokuwa kikiendelea uwanjani hapo.Waimbaji walikuwa wengi sana kutoka Iringa na

Wednesday, July 23, 2014

AMBWENE MWASONGWE, MESS JACOB CHENGULA NA WENGINE WENGI KUWASHA MOTO KATIKA UZINDUZI WA MWANADADA FURAHA ISAYA JUMAPILI HII

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxrmAYx1QLdTjnYEIESgH1yk-h9gllEoE1EL5tvNVWnZ2H_68Gw5t6WM9z_Uze_s0VCSoM-Kcrsi91vpON_yKnZSXoPusm0kRHL5NeixPddKjvuHLrH2KufYGwBgN0FkgZJWs76Au79rpd/s400/ambwene.JPG
 Waimbaji zaidi ya 20 kuvamia jukwaa moja wakitumia mic moja katika uzinduzi wa albamu moja ya mwimbaji mmoja siku moja na katika ukumbi mmoja akiwemo mgeni rasmi

JESUS IS NOT COMMING BACK - ROMAN CATHOLIC LEADERS SAID



A SPOKESPERSON for the Vatican (Roman Catholic) has officially announced today that the second coming of Jesus, the only son of the God, may not happen now after all, but urged followers to still continue with their faith, regardless of the news.

Cardinal Giorgio Salvadore told WWN that this years 1,981st anniversary is to be the Vatican’s last in regards to waiting for the Lord to return to Earth.

“We just feel Jesus is not coming back by the looks of it.” he said. “It’s been ages like. He’s probably flat out doing other really good things for people somewhere else.”

Nearly two thousand years ago, Jesus promised his disciples that he would come again in chapter John 14:1-3 of the bible: “There are many homes up where my Father lives, and I am going to prepare them for your coming. When everything is ready, then I will come and get you, so that you can always be with Me where I am. If this weren’t so, I would tell you plainly”

The Vatican defended Jesus’ broken promise, claiming “he was probably drinking wine” at the time when he made the comments.

“Having the ability to turn water into wine had its ups and its downs.” added Cardinal Salvadore. “We all make promises we can’t keep when we’re drunk. Jesus was no different.”

The church said it will now focus attentions on rebuilding its reputation around the world, but will keep an optimistic mind for the savior’s second coming.

Source: EACVISION

PAMOJA NA KEBEI NA KUZOMEWA MCHUNGAJI STELLA AENDELEA KUHUBIRI INJILI

Mhubiri wa Injili ambaye ni mama aliyejitambulisha kwa jina la Stella Mahiga amejikuta akipata wakati mgumu alipokuwa anahubiri majira ya jioni katika kituo cha kupandia daladala kilichopo Kariakoo jijini Dares salaam.
Aidha, mhubiri huyo aliyekuwa anahubiri kuhusu wokovu amejikuta akizomewa na watu aliokuwa akiwahubiria injili katika eneo hilo. Asilimia kubwa ya watu walikuwa katika hilo walikuwa ni wa dini nyingine.
Mpaka mwandishi wetu anaondoka katika eneo hilo aliacha wananchi wakiwa wanamzomea mhubiri huyo kwa maneno ya kejeli. Kwa ujumla hajapata ushirikiano hata kidogo kutoka eneo hilo, lakini Neno litaendelea kuhubiriwa.


Mchungaji Stella Mahiga akiendelea kuchapa injili maeneo ya k/koo

Huku akiendelea kuhubiri, huku akizomewa na kundi la watu

USEJA WA MAPADRI SASA KATIKA MJADALA, WANAWAKE NAO RUKSA KUWA MAASKOFU

Wimbi la mabadiliko hayo limeyakumba makanisa hayo mawili baada ya viongozi wao wakuu kulazimika kufanya maamuzi mazito juu ya mapadri na maaskofu wanaoyatumikia , ambapo tayari wanawake wameruhusiwa kuwa wachungaji na maaskofu, huku suala la mapadri kutoruhusiwa kuoa likipata ruksa ya kujadiliwa.


Wimbi hili la mabadiliko limekuja wakati mmoja, ambapo kwa upande wake kanisa Anglikana tayari limeruhusu rasmi wanawake kuwa wachungaji na maaskofu , wakati kanisa katoliki nalo limeruhusu mjadala juu ya ama mapadri wake waendelee na utaratibu wa kutooa au waoe.
Vyombo vya habari vilielezea tukio hilo kama moja ya matukio makubwa katika karne ya 21 kwa kanisa Anglikana, lililoanza tangu miaka 20 iliyopita na hatimaye kukamilika hivi karibuni.
Shirika la habari la kimataifa la sky News limemkariri Askofu Welby akisema kuwa amefurahishwa sana na matokeo ya kura hizo na kwamba ni mwanzo mzuri wa shughuli kubwa ijayo.
Nayo Televisheni ya kimataifa ya CNN katika moja ya vipindi vyake vilivyoripotiwa juu ya tukio hili ilibainisha kwamba huenda kanisa Anglikana likawa na maaskofu wengi wanawake kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.

Source: Strictly Gospel

VIUNGO VYA BINADAMU VYAKAMATWA DAR ES SALAAM LEO ...ANGALIA PICHA HAPA

Jamani dunia inaenda wapi sasa? Mbona majanga mengi sana? Kila kuitwapo leo mambo mabaya wanazidi kuongezeka. Kama Wakristo tunatakiwa sasa kusimama na kuomba juu ya hili tukio la kinyama. Taifa la Tanzania sasa tupige magoti mbele za Mungu na kutubu dhambi zetu na dhambi za wengine. Watu wamekuwa wanyama na kuwa na roho za ukatili wa kufikia kiwango cha kuua wanadamu wenzao.

Tumesikia mengi juu ya mauji yanayonyanyika mitaani mwetu, ya kwamba asilimia kubwa ni kwaajili ya kujipatia fedha na wengine katika imani ya kisheti za kutomwamini Mungu bali kumwamini mwanadamu na kumtumikia. Watu wanauana ili wapate fedha kwa njia hata ushirikina.

Jamani tuone taarifa kuhusiana na mauaji hapo chini:-

Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili

ALBAMU YA "NAHITAJI KITU GANI" KANISA LA KIJITONYAMA LUTHERANI LATIKISA WANA DAR ES SALAAM

Waumini ndugu jamaa na marafiki waliofika katika kanisa la Kilutheri usharika wa Kijitonyama jijini Dar es salaam, walipata wasaa mzuri wa kumsifu Mungu pamoja na waimbaji mbalimbali waliofika kumsindikiza Oliver Israel mwimbaji wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambaye alikuwa akizindua kanda yake ya kwanza ya sauti.

Israel akienda sambamba na mkewe.

Tendo la uzinduzi lilianza katika ibada ya kwanza na kuendelea ibada ya pili na kuhitimishwa wakati wa tamasha kubwa majira ya mchana ambalo mgeni rasmi mwalikwa alikuwa meya wa manispaa ya Ilala bwana Jerry Slaa ambaye alionyesha kufurahia tukio zima la uzinduzi wa album hiyo inayofahamika kwa jina la 'Nahitaji Kitu Gani?'.

Oliver ambaye alipendeza haswa kwa mavazi aliyokuwa amevaa alishikiana vyema na mumewe bwana Israel Mujumba ambaye pia ni mwimbaji na mpigaji wa kwaya ya Kijitonyama, alikuwa akimwitikia mkewe katika uimbaji huo akishirikiana na waimbaji wengine wa kwaya hiyo.

Chini ni baadhi ya picha za uzinduzi huo.

Mheshimiwa meya wa manispaa ya Ilala Jerry Slaa akizindua CD hiyo.

Oliver akimshambulia shetani.

Ilikuwa safi kabisa.

Kucheza nyumbani mwa Bwana raha.

Hakika alipendeza na kazi ilifanyika.

Saturday, July 12, 2014

MKURUGENZI WA RUMAFRICA RULEA SANGA AMEFIWA NA SHEMEJI YAKE MBEYA USIKU

Rulea Sanga ambaye ni mkurugenzi wa blogu hii siku ya jana akiwa na masikitiko makubwa sana baada ya kupata taarifa kutoka kwa mtoto wa kaka yake, Furaha Sanga usiku wa kuamkia  jumamosi 12/07/2014 ya kwamba shemeji yake aliyekuwa akimuuguza Muhimbili amefariki dunia.

Rulea Sanga baada ya kupata habari za kifo cha shemeji yake nyumbani kwake Sinza

Mgonjwa huyo ameugua kwa muda mrefu kidogo kwa ugonjwa wa kansa ya mifupa na koo. Ugonjwa huu ulimtesa sana na mpaka ikalazimika kumleta Muhimbili Dar es Salaam. Hali ake ilizidu kuwa mbaya kila kuitwapo leo, na mwisho wa siku madaktari wakaamua kumruhusu aende nyumbani kwani ilionekana ni ngumu sana kumtibu.

Wanafamilia walilzimika kumsafirisha mgonjwa mpaka mkoani Mbeya ambako ni nyumbani wa marehemu. Na leo hii amefariki dunia.

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA JUBILEI YA MIAKA 75 YA TAG TANZANIA YALETA NEEMA MKOA WA MBEYA.

KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) nchini linaadhimisha sherehe za miaka 75 tangu kuzaliwa kwake zinazofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.

Kutokana na maadhimisho hayo Jiji na Mkoa wa Mbeya utanufaika na sherehe hizo kutokana na shughuli ambazo Kanisa hilo litafanya katika siku zote za maadhimisho hayo.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Askofu Mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali, katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa MMRP jijini hapa, alisema Sherehe hizo zitaambatana na shughuli mbali mbali.

Askofu Mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa MMRP jijini hapa.

Alisema maadhimisho hayo yatafikia kilele Julai 13, Mwaka huu katika sherehe zitakazofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Dk. Jakaya Kikwete Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Askofu alisema kabla ya sherehe hizo kutakuwa na zoezi la kugawa vyandarua 8550 vyenye thamani ya shilingi 270 kwa ajili ya Hospital,Vituo vya Afya pamoja na zahanati zinazo laza wagonjwa katika Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Njombe.

Askofu Mtokambali alisema mbali na kanisa kutoa msaada wa Kiroho kwa waumini wake lakini limeona katika kushurehekea miaka 75 ya tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo hapa nchini ni bora wakafanya na huduma za kijamii.

Askofu Mtokambali alisema vyandarua vitagawiwa katika Hospitali 34 na vituo vya afya 83 katika mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa zoezi litakalofanyika kuanzia Julai 1 hadi julai 4, Mwaka huu.

Alisema katika mgawanyo huo vyandarua 1300 vitaenda Mkoani Rukwa katika Hospitali 3 na vituo vya afya 22, Mkoa wa Njombe vyandarua 3100 kwa ajili ya Hospitali 11 na vituo vya afya 25.

Askofu alisema Vyandarua 4150 vitabaki Mkoa wa Mbeya katika Hospitali 20 na vituo vya afya 36 ambapo kati yake Vyandarua 500 vitabaki katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Vyandarua 150 vitakua kwa ajili ya Hospitali ya Wazazi ya Meta.

Mbali na msaada wa vyandarua Askofu Mtokambali alisema pia kanisa hilo litaendesha zoezi la uchangaji damu litakalowagusa Wachungaji zaidi ya 800 hivyo kupunguza upungufu wa damu unaokikabili kituo cha damu salama Kanda ya Mbeya.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Husein Kandoro, alipokea vyandarua 650 kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo kati yake vyandarua 150 vitagawiwa katika Hospitali ya Wazazi ya Meta.


Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Husein Kandoro, alipokea vyandarua 650 toka kwa Askofu mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali,

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abasi Husein Kandoro akishukuru msaada huo kwaniaba ya Hospitali ya rufaa




Dr. Leonard Maboko Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ya TAG ambae pia ni Mkurugenzi wa NIMR, akitoa neno kwa wageni

Kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dr. Kaimu Mku Humphrey Kihwelu akimkaribisha mkuu wa mkoa Mbeya









TUMUOMBEE NDUGU YETU ORIDA NJOLE

Kwa wale wasiomjua Oride Njole, ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Leo hii yuko kitandani anaumwa, anatamani kuwa kama wewe ambaye kwa sasa unacheka na kufurahi lakini anashindwa kutokana na ugonjwa alionao. Jamani ndugu yetu anaumwa sana tunapaswa kumuombea na ikiwezekana tufike pale hospitalini Temeke hospitali ya serikali.


Orida Njole

RUMAFRICA YAPATA TAARIFA ZA UGONJWA

Rumafrica imepokea habari hizi siku ya leo kwa njia ya simu kutoka kwa mtangazaji wa Radio Tumaini Obedi Kikao, anasema hali yake sio nzuri sana, ndugu yetu anateseka sana. Kama binadamu mwenye huruma basi fika pale hospitalini kumpa pole ndugu yetu huyu. Kumbuka ulikuwa naye kipindi mnacheka leo hii mwenzetu amenuna kutoka na maumivu anayopata. Anahitaji faraja kutoka kwako Mtanzania.



NDUGU NA MARAIKI
Kumbuka wewe rafiki uliyekuwa unacheza naye mpira wa mikono, Oride ni mwanamichezo mkubwa sana na amekuwa nawe katika michezo mbalimbali, lakini leo hii anashindwa hata kushika mpira kutoka na ugonjwa alionao. Umefika wakati wa kwenda kumuona ndugu yetu na kubwa zaidi ni maombezi.


WACHUNGAJI NA WATUMISHI WA MUNGU

Mchungaji ambaye ulikuwa ukimtumia Oride Njole katika huduma yako, ameimba sana kanisani kwako lakini leo hawezi kuimba tena kutoka na kile kinachomsumbua. Nenda basi ukamuombee pale kitandani alipolala ili aweze kuamka na kufanya kazi ya Mungu kama zamani. Kuwa na moyo wa huruma basi.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpcMsU4UDDl4vIXd1MwP8MvUId48K_ikpQWGd22kMhWCt5YBYc5VGrLzv0liokXFbDFMznaTUy6wuqSS2A8-DMybXem8z4lqODP_-yQadnh3WjwBlxr7zYO6zzicpMUIGVQZsQzyxRc44/s640/orida6.jpg
Orida Njole akimtumika Mungu kanisani

Hata wewe mchungaji ambaye unayemfajhamu na wewe uliyemfahamu kwa kupitia blogu hii ya Rumafrica basi acha hicho unachofanya sasa anza kumuombea. Ondoa hiyo roho inayokusukuma usimmuombee na ikemee sasa.

WANAMICHEZO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjFCSx2bexVJA9Wah14-vk1c8v53ZdG5hQYg0Ap36u_yLGHwruJa9AzpkUrm5LieZhIYOhpTfEODic15xpiZtihpc3fWQa45lkL6J7ZA9yshkYPJTGTtYhNTQef3NPqmd1y6QoO5nwjtlM/s640/DSCN7837.JPG
Orida Njole (kushoto)

Marafiki zake ambao mmekuwa naye studi kurekodi nyimbo za kumtukuza Mungu, sasa tunawaomba mfanye maombi na kufika pale hospitalini kumtia moyo na kumpa pole. Mmekuwa mkicheka na kupeana mawazo studio lakini leo hii mwenzenu anashindwa hata kuwapa mawazo kutokana na maumivu anayopata. Kuwa na moyo wa upendo na huruma kama vile mnavyotuimbia sisi tuyafanye yale manyoimba.
http://photos-a.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-ash3/t1.0-0/c0.2.960.639/s720x720/379618_192151074260838_1925803444_n.jpg
Orida Njole kushoto wa kwanza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOc94V7rzBA9MjQnGXUfMkwNyCilQehUIwRe0pYcKCpmy_beUlXaIlMtBQY9UEDUyrOAtBmTQCOnOfEHz8ivLDzZYOA4yt7vrx1qz0MiWB9lMADlaSeumb09fA_X-qKeOBPhO4px8yThPE/s640/Orida-Njole-Poster.jpg
DVD Cover la albamu ya Orida Njole

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEio7m648oQfHoZQ0qJ8Tifc95KheVfeAkkTLODt8BEDVFI_zBUE69mYsI7lu0WDjuJgr2nydTcOTwwAxL3thucieY8ifpOOeJdQtqZq6_AlzYPC46Ut9-2BaPskWiSO6R0C1MuvZGR0GRoo/s640/Orida.jpg
Orida Njole

MATUKIO KATIKA PICHA:WINGU JEUSI LATANDA MSIBA WA SISTA ANNA, DAYOSISI YA KUSINI

Msiba wa sista Anna Peterson umeibua simanzi si kwa familia yake tu bali kwa wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe alipokuwa akifanya kazi za kijamii tangu ujana wake.

Hayo yamebainika wakati wa ibaada maalum ya kumkumbuka iliyofanyika hii leo katika kanisa la KKKT usharika wa Amani Bulongwa, ibaada iliyoongozwa na baba askofu wa dayosisi ya kusini kati Levis Sanga, Askofu Mstaafu Dkt. Solomon Swallo na Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa pamoja na msaidizi wa askofu Philemon kahuka.


Sista Anna Enzi za uhai wake.

Akihubiri katika ibaada hiyo maalum Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa amesema marehemu alikuwa akifanya kazi zake kwa mkono wa dayosisi ya kusini kati tangu enzi za ujana wake bila ubaguzi ingawa yeye alikuwa mzaliwa wa nchi ya Sweeden.

Amesema amemfahamu toka 1969 na hadi anafikwa na umauti alikuwa akisaidia watoto yatima, wajane, wagane na walemavu wote na hata wasiojiweza na kusisitiza kuwa kanisa haliwezi kumsahau kamwe.

Akielezea historia ya marehemu Askofu mstaafu Dkt Solomon Swallo amesema Sista Anna alikuwa akifanya kazi zake kwa kujituma bila kujali ugumu wa kazi uliokuwepo kwa kipindi hicho hasa ubovu wa barabara na ugumu wa kuwafikia wananchi kutokana na tabu ya usafiri.

Askofu mstaafu Manyiewa akihubiri ibadani hapo.

Dkt Swallo amesema alikuwa akisisitiza kuwa Mungu ndiye aliyemtuma kufanya kazi Bulongwa Makete na si Binadamu hivyo haoni shida kutumikia jamii ya Makete toka ujana hadi uzee wake.

Askofu mstaafu Dkt Solomon Swallo.


Dkt Nicodemas Kikoti.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu hospitali ya Bulongwa Dkt Nicodemas Kikoti amesema marehemu pia alikuwa akifanya kazi na hospitali hiyo pamoja na jamii ikiwemo kusomesha watoto yatima kutoka shule ya awali mpaka vyuo, kuwajengea nyumba wasiojiweza, kuhudumia wajane, kusaidia vifaa vya umeme pamoja na kujenga makao ya kituo cha watoto yatima Bulongwa.


Mch. Dkt Phares Ilomo.

Naye Mch. Dkt Phares Ilomo kutoka chuo Kikuu cha Iringa amesema yupo tayari kuandika kitabu cha kuelezea historia ya marehemu Sista Anna kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kanisa na washarika kuchangia gharama ili kitabu hicho kichapishwe na kuzalishwa kwa faida ya vizazi vijavyo ikiwemo kukiweka katika maktaba ya chuo chake.

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mahenge ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Makete akitoa salamu za rambirambi amesema marehemu alikuwa akifanya shughuli ambazo kimsingi zilitakiwa kufanywa na serikali hivyo wema wake kwa jamii ya Makete hauna mfano.


Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mahenge ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Makete akitoa salamu za rambirambi.

Amesema njia pekee ya kumuenzi ni kufanya yale aliyoyapenda huku akisisitiza kuwa serikali itashirikiana na kanisa kuendeleza kazi zote alizoziacha Sista Anna.


Askofu wa dayosisi ya kusiki kati Levis Sanga.

Askofu wa dayosisi ya kusiki kati Levis Sanga ametangaza tarehe 26 Juni kila mwaka kuwa ni siku maalum kikanisa ya kumkumbuka marehemu sista Anna hivyo jamii inashauriwa kufika kwenye kituo cha watoto yatima Bulongwa kwa ajili ya kuwatembelea na siku hiyo itakuwa ikifanyika ibaada maalum kwa ajili ya marehemu.

Sista Anna Peterson amefariki Juni 26 mwaka huu nchini Sweeden alipokwenda kwa ajili ya matibabu na amezikwa leo hii nchini humo, na hapa Makete alikokuwa akiishi toka ujana wake imefanyika ibaada maalumu ya kumkumbuka.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Sista Anna Peterson, Amen.

Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete

ASKOFU MKUU WA TAG AWAONGOZA WACHUNGAJI KUCHANGIA DAMU

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali amewaongoza wachungaji zaidi ya 800 kuchangia damu.
Askofu alisema uchangiaji damu huo ni moja ya adhima ya kanisa ili kukabiliana na upungufu wa damu unaokikabili kituo cha damu salama kanda ya Nyanda za juu kusini hivyo litaendeshwa kwa muda wa siku tatu kuanzia Julai 10 hadi 12,mwaka huu ili kukamilisha wachungaji zaidi ya 1000 nchi nzima.
Alisema kama kanisa na Viongozi wameguswa na tatizo la upungufu wa damu katika mahospitali kutokana na watu kupata ajali kila siku, wanawake kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua pamoja na watoto ndiyo maana wakaona ni vema wakaonesha mfano wa kuchangia damu.
Aidha alitoa wito kwa viongozi wengine wa dini bila kujali itikadi zao kuchangia damu popote pale walipo ili kuokoa maisha ya Watanzania wenye mahitaji kwa kuwa damu haiuzwi na hakuna kiwanda cha kuzalisha zaidi ya mtu kujitolea.
Kwa upande wake Afisa tabibu wa Damu Salama kanda ya Nyanda za juu kusini yenye makao makuu katika Hospitali ya Wazazi Meta jijini Mbeya, Alex Kasimba,alisema ni kweli kuna upungufu mkubwa wa damu katika Benki yao.

Alisema kwa takwimu za Mwaka jana damu iliyokuwa ikihitajika ni chupa 28000 lakini Benki ilifanikiwa kukusanya chupa 19000 sawa na asilimia 68 hivyo kuwa na upungufu wa chupa 9000 sawa na asilimia 32.
Alisema hata mwaka huu wanauhitaji wa kiasi kama hicho ili kuweza kuziba pengo la upungufu wa damu ambapo kupitia maadhimisho ya Miaka 75 ya TAG wanatarajia kukusanya zaidi ya Lita 400.
Aliongeza kuwa taasisi za kidini kama TAG, Sabato, Waislam na taasisi za elimu kama Shule za sekondari na vyuo ndiyo wanaojitolea kwa wingi damu tofauti na wananchi wa kawaida.
ASKOFU mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali akichangia Damu
Baadhi ya wachungaji wa kanisa la TAG wakitoa damu na wengine wakisubiri zamu yao

ASKOFU mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali akipimwa Damu
Makamu Askofu Mkuu, Dk. Mhiche akipimwa damu kabla ya kutoa
Baadhi ya wachungaji wengine wakiwa katika foleni ya kujiandikisha kutoa Damu

ASKOFU mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas akiongea na waandishi wa habari
 Afisa tabibu wa Damu Salama kanda ya Nyanda za juu kusini yenye makao makuu katika Hospitali ya Wazazi Meta jijini Mbeya, Alex Kasimba akiongea na waandishi wa habari
Anthony Damas mwandishi wa apostledarmacy.blogspot.com
Zoezi hilo liefanyika katika Chuo cha Biblia kilichopo Itende jijini Mbeya ambapo Askofu huyo katika kuonesha uzinduzi na yeye alichangia.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchangia, alisema Wachungaji wameona wachangie damu kutokana na upungufu na mahitaji yanayoikabili Benki ya damu salama.
Alisema katika zoezi hilo ni wachungaji 800 ambao ni waangalizi wa kanisa ndiyo watakaoanza kuchangia na kufuatiwa na wachungaji wote kutona nchi nzima ambao watakuwepo mkoani Mbeya kwenye maadhimisho ya miaka 75 ya TAG.